Tuesday, 20 May 2014

WARAKA WA MRAP (LION) KWA MASHABIKI ZAKE.





Mpendwa Shabiki wangu, shabiki wa
Mrap Lion. Napenda kuchukua nafasi
hii kumshukuru MUNGU, wewe
SHABIKI wangu na mtangazaji bora na
mahili kabisa hapa nchini dada yangu
“Fetty” ndani ya “SO SO FRESH” inayopatikana
hapa kwenye Radio ya
watu CLOUDS FM.

Siku zote katika maisha yangu
tokea
nimeanza kazi ya muziki, nimekua na
shauku kubwa sana kutaka FANS
wangu muweze kunijua na kujua kila
kitu ninachokifanya katika maisha
yangu hata ikiwezekana kila siku iendayo kwa
mungu kuweza kuona
Mrap Lion anafanya nini, lakini nafasi
ni ndogo sana ila ntatumia nafasi hii
kuweza kukuweka karibu wewe
shabiki yangu sababu najua hamu
yako kutaka kujua MRAP anafanya nini.

Naitwa “Richard Alibalio Prudence” also known as, Mrap
Lion, mzaliwa wa jijini Dar Es Salaam katika
hospitali ya
Muhimbili. Nimepata elimu yangu
katika mikoa tofauti nchini Tanzania
ikiwemo Kagera, Zanzibar na Dar katika shule za
Rubya Seminary – Kagera, Francis Maria Secondary
School – Zanzibar na Jitegemee High School –
Dar, nilipomalizia elimu yangu ya sekondari na sasa
nipo chuo
cha usimamizi wa fedha (IFM) mwaka wa kwanza
nikichukua “Bachelor Degree of Insurance and Risk
Management”

Nimeanza kufanya kazi zangu za
muziki mwaka 2010 kipindi nipo
elimu ya sekondari na kufanya kazi na
studio za mtaani na kufikia kufanya
kazi na studio kubwa zikiwemo AM Records chini
ya Producer Manecky na Bob Manecky, BHitz
studio inayomilikiwa na Producer Hermy B chini ya
Producer Pancho Latino ambae aliniona kwenye
nyimbo
niliyofanya na Makamua chini ya Producer Manecky
ijulikanayo kama “Tunamaintain”. Baada ya
kufanya kazi na studio hizo hivi sasa nafanya
kazi zangu mwenyewe chini ya
usimamizi wa aina tofauti kabisa na
kazi nyingi za aina tofauti
zimeshafanyika na tunaendela
kufanya zaidi kwa ajili ya nyie Fans wangu ambao
naamini kabisa kila
ninachofanya ni kwa ajili yenu.

“MRAP LION” ni jina
lililotokana na majina yangu mwenyewe binafsi
niliyopewa na wazazi wangu ambapo ‘M’ inatokana
na “Mwijage”, ‘R’ Richard, ‘A’ Albalio, ‘P’ Prudence
na LION imetokana na NYOTA yangu
“LEO” (SIMBA) sababu nimezaliwa tarehe 18 mwezi
wa 8 (August).

Kama msanii chipukizi wa muziki
wa
kizazi kipya ujulikanao kama “Hip
Hop”, kuna vitu vingi sana na mipango
endelevu kimuziki huku nikiendelea
na masomo yangu. Mwaka huu wa
2014 kuna mipango mingi sana kwa kudokeza tu
kuwa nje ya usanii wa
muziki vile vile nimeanza kufanya kazi
kama ‘Actor’ ambapo nimeshafanya
‘Short Film’ ambayo ni kwa ajili ya
mafunzo kwa jamii katika mlengo wa
utumiaji wa madawa ya kulevya. Madawa ya
kulevya kwa sasa
yanahatarisha maisha ya vijana wengi
hapa nchini na ambao ndio Taifa la
kesho la Tanzania. Filamu hii imenuia
na madumuni yake ni kulenga
wanafunzi wa Nyanja tofauti ambao ndio wenye
nguvu na tegemeo la taifa
la kesho la nchi yetu, uzinduzi wake
pamoja na mipango iliyopangwa
katika shunguli hii itawalenga
wanafunzi kuanzia ngazi ya
Sekondari. Mengine zaidi ya kazi hizi yatawajia
zaidi wakati muafaka.

Mwisho kabisa napenda
sana
kushukuru mashabiki wangu (Fans)
sababu kama nilivyosema mwanzoni
bila nyinyi siwezi kuwa Mrap LION
anaeandika barua hii kwenu, nipo
kwa ajili yenu na hakuna siku ambayo nitakuwa
mimi bila nyinyi, nashukuru
sana sana kwa support mnayonipa
tokea nimeanza mpaka hivi sasa, sister fetty, So So
FRESH na CLOUDS MEDIA GROUP, Madj, bloggers
na wengine wote katika Media na Entertainment
mnaofanya kazi ya kusaidia muziki
wangu kuwafikia Fans wangu popote
pale walipo. ASANTENI SANA.

GOD Bless You ALL

MRAP LION




  • CREDIT:GONGA MX.

No comments:

Post a Comment