KIFO cha nyota wa filamu Bongo, Adam
Kuambiana kilitibua sherehe ya kumbukumbu ya
kuzaliwa ya watoto wawili Nicole na Martin
iliyoandaliwa na Aunt Ezekiel akiwa na shoga
yake Wema Sepetu.
Mastaa hao walikuwa wamekamilisha kila kitu
na walishaanza shamrashamra zaa, ghafla
wakasikia taarifa za kifo cha Kuambiana.
Aunty Afunguka
“Mi naumia jamani, unajua filamu yetu ya
mwisho tuliyocheza mimi na Wema, yeye alikuwa
dairekta. Yaani tulikuwa tukimchezea kama babu
yetu, hebu angalia hii clip,” alisema Aunt huku
akimwonyesha mwandishi wetu clip hiyo kwenye
simu yake.
Hata hivyo kwa kuwa walikuwa
wameshatayarisha kila kitu huku waalikwa
wakiwa eneo la tukio, walimalizia hafla hiyo
ingawa machozi yakitawala badala ya furaha
CREDIT:GPL.
No comments:
Post a Comment