Official fan blog "Classmate" is one among Bongo Classmates properties... It's all about reporting of Current affairs..
Sunday, 25 May 2014
SIFA KUU TANO ZA MWANAMKE ZIPENDWAZO NA WANAUME.
1. Mwanamke anapaswa kuwa na
maisha yake na sio maisha ya kuiga.
Wapowanawake ambao hupenda kuiga
kile kinachofanywa na wanawake
wenzake na kudhani hivyo ndivyo
anavyopaswa kuwa. mwanamke
mwenye tabia hiyo huwa hana mvuto
kwa mwanaume kwani atakuwa ni
mwana mke fake.
2. Mwanamke anapaswa kuwa mtiifu na
mwenye heshima na pia mwenye
busara. Mwanamke hapaswi kuwa na
kiburi na kutaka kuota mapembe ndani
ya mahusiano. Heshima na utiifu
haimaanishi kuwa tayari kunyanyaswa,
hapana. Mwanamke anapaswa ampe
mpenzi wake ama mumewe heshima
inayotakiwa kama kichwa cha
mahusiano yenu.
3. Mwanamke anapaswa kuwa na uwezo
wa kujitegemea. Hapa utata idogo, wapo
wale wanaoamini kuwa mwanamke
anapaswa kutegemea kila kitu toka kwa
mwenza wake. lakini ukweli ni kwamba
wanaume wengi wanapenda kuwa na
uhusiano na mwanamke ambaye
anaweza kusimama kwa miguu yake na
kujitegemea pia.
4.Mwanamke lazima awe anajiamini.
Naam, hapa haimaanishi kuwa
anatakiwa kuwa kiburi na
mbishi hapana. Isipokuwa mwanamke
anapaswa aonyeshe kujiamini kwa kile
anacosema na anachotenda. Kujiamini
kunamfanya mwanaume ajue kuwa ana
mpenzi ama mke ambaye anaweza
kukabiliana na mikwaruzo mbalimbali
inayohitaji hoja na utetezi.
5. Mwisho, mwanamke anapaswa kuwa
na mvuto. Hapa haimaanishi kuwa
mrembo saaaana, hapana. Ina maana
kuwa mwanameanapaswa kuwa nadhifu
kila wakati ili kumfanya mwanaume
apende kuwa nawe na avutiwe kuwa
nawe wakati wote. Sifa hizi tano akiwa
nazo mwanamke, basi atambue fika
kuwa Mwanaume atavutiwa nawe na
uhusiano wenu unaweza kudumu na
kudumu na kudumu.
Labels:
Above 18
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment