JACK WOLPER
Mrembo kutokea kwenye kisima cha uigizaji Tanzania ,Bongo movie maarufu kama Jack Wolper akiri kutowahi kulia pindi aachwapo na mpenzi wake yoyote yule.
Akizungumza na mwanahabari wetu, Wolper
ambaye ana muonekano wa ‘kigumu’, alisema
siku zote anaamini katika kupambana hivyo
hawezi kumlilia mwanaume hata iweje.
“Sijawahi kulia pale nilipoachwa wala kuachana
na mwanaume, akili yangu yote inaamini katika
kutafuta maisha hivyo siwezi kujirahisisha
nikamwaga machozi kwa ishu za mapenzi,”
alisema Wolper.
Credit:Pamojasisi blog
No comments:
Post a Comment