Official fan blog "Classmate" is one among Bongo Classmates properties... It's all about reporting of Current affairs..
Friday, 23 May 2014
FID Q AMPA MAKAVU DAYNA KUHUSU UTUMIAJI WA MKOROGO.
Kutokana na sababu ambazo zilikua nje ya
uwezo hukusikiliza You heard ya juzi Mei 20
sikuiweka hapa ,sasa kwa kuwa nipo kwa ajili
yako na sipendi upitwe na kitu,You heard ya jana
ilikua inamhusu Fid Q na Dayna na Fid Q
ameingia hasa utata wa kwenye line zake
kadhaa kwenye wimbo wa Sina Muda wa Jcb
ambazo zimeonekana kumhusu moja kwa moja
Dayna.
Fid Q ameonekana kama anamfokea Dayna kwa
kutumia mkorogo unao badilisha ngozi yake na
kuonekana mweupu kitu ambacho Fid Q amedai
kuwa Dayna anaukimbia uafrika,Mistari ya Verse
hiyo iko hivi.
“Hi Dayna, sikufichi ulikua unahusika/
au mtoto wa uswazi ‘ akijichubua ‘ haimaanishi
anaukimbia uafrika?/
nisikize Dayna..please.. najua uko busy kiaina na
hizi ni aina tu za uchizi au kama vipi bye DAYNA/
HUUH.. now back to you fools/
Soudy brown kamtafuta Fid Q ambapo alipoulizwa
kuhusu hili majibu yake alidai kuwa katika ngoma
hiyo hamzungumzii Dayna Msanii bali
anamzungumzia Dayna msichana anayeishi nae
kitaani maeneo ya Mikocheni kwa Nyerere.
Dayna huyo wa kiafrika alikua mweusi sasa hivi
amejichubua ngozi yake na kuwa mweupe
ambapo baadae Fid Q aliuchambua kiutaalam
mstari huo na kusema kuwa wadada wanaofanya
hivyo wanaua melanie.
Ambacho ni kitu muhimu sana kwenye ngozi na
hupatikana zaidi kwenye ngozi nyeusi ya kiafrika
chembechembe ambazo huilinda ngozi isiunguzwe
na jua.
Majibu ya Dayna baada ya kupigiwa simu na
Soudy Brown kutaka kujua kama ameshaisikia
hiyo line ya Fid Q alichokijibu ni ameisikia na
anamuheshimu Fid Q kwa wazo lake ila kwa
wakati huu amepunguza kidogo kutumia
mikorogo.
Labels:
Bongofleva,
Dayna,
Fid Q
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment