Sunday, 25 May 2014

DIVA AKUBALI KUSHOOT VIDEO AKIWA NUSU UCHI NA DIRECTOR WA KENYA.


Diva The Bawse ambaye ametoa wimbo
wake mpya ‘Mashallah’siku chache
zilizopita, amesema anajiandaa
kuufanyia video pamoja na kuanza tour
ya kuutangaza wimbo huo.
“Video tunatarajia kufanya na aliyefanya
‘Asante’ ya Ay,” Diva ameiambia
Mpekuzi leo.
Ameongeza kuwa kwasasa ameamua
kuingia kwenye muziki kwa miguu yote
miwili, ndio sababu anatarajia kuanza
kufanya tour mikoani kuutangaza
wimbo wake.

“Nahitaji kutumia muda mwingi
kuutangaza huu wimbo, ambao uko chini
ya management ya Sharobaro Recs, na
ningependa kuulizwa maswali
yanayohusu muziki zaidi kuliko mambo
binafsi, nahitaji kuwa na privacy na ku-
focus na biashara yangu, maisha yangu
ya radio na muziki.” Alisema Diva  na
kuongeza
“Pia nina meneja mpya anaitwa Kerry
Kerwin ambaye anamsimamia Victoria
Kimani akiwa hapa Tanzania, na pia
niko tayari kuanza kufanya shows za
mikoani. Tutahakikisha huu wimbo
unafika katika radio zote za mikoani
Tanzania na nje, na habari njema ni
kuwa ‘Mashallah’ imeanza kupigwa
Nairobi.”

No comments:

Post a Comment