Official fan blog "Classmate" is one among Bongo Classmates properties... It's all about reporting of Current affairs..
Tuesday, 27 May 2014
SALMA JABU(NISHA) AMWAGIWA MATUSI YA NGUONI CHANZO KIKIWA NI MWANAUME.
Matusi! Staa wa sinema za Kibongo, Salma Jabu
‘Nisha’ amejikuta kwenye wakati mgumu baada
ya kutukanwa matusi ya nguoni na mwanadada
anayejulikana kwa jina la Muna Alphonce kisa,
kikidaiwa ni mwanaume.
Habari ya mjini ilieleza kwamba Muna ambaye ni
mke wa mtu aliporomosha matusi ya nguoni
ambayo hayaandikiki gazetini huku akimtoa
kasoro mbalimbali Nisha na kumweleza kuwa
hakuwahi kufikiria wala kuwa na uhusiano wa
kimapenzi na mpenzi wake wa sasa kwani ana
mume na familia.
“Sina uhusiano na mwanaume wa Nisha ila kuna
siku moja alinipigia simu na kujitambulisha
kwangu kwamba anahitaji tufanye biashara
kwani anafanya biashara ya magari lakini
nikampotezea, akarudia tena mara ya pili pia
nikampotezea lakini sasa nashangaa Nisha kudai
ninamtaka mwanaume wake. Wewe nisha nikome
kabisa,” alisema Muna.
Baada ya kuzinyaka habari hizo na matusi hayo
ya nguoni, gazeti hili lilimtafuta Nisha na
kumuuliza kulikoni ambapo alikuwa na haya ya
kusema:
“Mimi sigombei mwanaume na mtu. Mwanaume
wangu ninampenda na yeye ananipenda
japokuwa watu wanazungumza mengi,” alisema
Nisha.
Labels:
Salma jabu(nisha)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment