Sunday, 25 May 2014

JB AKANUSHA KUPIGANA NA STEVEN NYERERE.

Muigizaji wa filamu, Jacob Stephen aka JB
amekanusha tetesi za kupigana na mwenyekiti
wake Steve Nyerere kutokana madai ya
kuzungukana katika deal la matangazo.
Akizungumza na Bongo5 JB, amedai kuwa hawezi
kufanya kitu kama hicho kwani Steve Nyerere ni
mwenyekiti wake.







“Jamani mimi nimeshawaambia mimi ni mtu
mzima jamani, Steve Nyerere ni mwenyekiti na ni
mtu ambaye ninamuheshimu, hakuna kitu kama
hicho mbwa acheni mambo yenu, mimi ni mtu
mzima na familia, kwahiyo mambo kama haya
siwezi fanya, kwenye msiba mimi sijagombana
chairman wangu, nashangaa watu wanalikuza hili
suala. J
Jamani Steve Nyenyere ni kiongozi wangu,”
alisema JB kwa hasira.

Mtandao wa bongo movies pamoja na mingine
imedai kuwa baada ya mazishi ya muigizaji na
muongozaji wongozaji wa filamu marehemu Adam
Philip Kuambiana, JB na Steve Nyerere
wanadaiwa walishikana na kupigana kutokana na
kuzungukana katika mambo ya matangazo.


CREDIT:BONGO5 .

No comments:

Post a Comment