Friday, 23 May 2014

UZEE MWISHO CHALINZE.....BABU AFUMWA GESTI AKIMLA URODA BINTI (PICHA NA STORI NZIMA VIKO HAPA).

Amakweli dunia imekwisha! Watu wa Dar es
Salaam wanasema uzee mwisho Chalinze, Dar es
Salaam kila mtu baby, kauli hiyo ilitimia usiku
wa kuamkia Jumanne iliyopita baada ya mmiliki
wa Gesti ya GLP ya Mabibo Mwisho jijini Dar es
Salaam, Amos Makelle kunaswa kitandani usiku
wa manane na mfanyakazi wake aitwae Tina.




Babu Amos Makelle baada ya kunaswa akiwa
kitandani na mfanyakazi wake aitwae Tina
wakiwa tayari kuchepuka.


Bosi huyo na mfanyakazi wake walinaswa na
mchumba wa Tina aitwae Salum Mbonde
ambaye alipenyezewa umbeya huyo na mteja
mmoja aliyekodi chumba kwenye gesti hiyo kwa
ajili ya kufuatilia nyendo za wawili hao.
Baada ya mchumba wa Tina kupewa umbeya
huo kuwa wawili hao walikuwa katika harakati
za kuchepuka aliwawekea mtego na
kuwashirikisha waandishi wa Oparesheni Fichua
Maovu ‘OFM’ na askari wa doria.
BOSI ATOA SHINGO KUCHUNGULIA NOMA
OFM na mchumba wa Tina wakiwa wamelizingira
eneo la gesti hiyo mishale ya Saa 8:17 usiku
kukiwa kumetulia tuliii... mtonyaji aliyekodi
chumba kwa ajili ya kazi maalum aliwatumia
ujumbe mapaparazi wa OFM kuwa mzee Makelle
aliyekuwa kwenye chumba chake alitoa shingo
kama mara tatu na kuangalia kulia na kushoto
kama kulikuwa na mtu aliyemuona.




Babu Amos Makelle bada ya kufumwa akiwa na
mfanyakazi wake gesti.


APIGA HATUA ZA KUNYATA
Ilipotimu saa 8:31, Mzee Makelle akiwa tumbo
wazi na kipensi chake aliangalia tena kama
hakukuwa na noma, akachomoka chumbani
kwake fastafasta kwa hatua za minyato na
kuzama chumba namba 104 alimokuwa Tina.
SHAAABASH... WANASWA KITANDANI
Shaaabash... baada ya dakika chache OFM na
mchumba wa Tina walizama kwenye chumba
hicho na kuwakuta wawili hao wakiwa kitandani
huku Tina akiwa na nguo za ndani.
Walipohojiwa na OFM Tina alikuwa akilia na
kumuomba radhi mchumba wake na kusema
bosi wake huyo ndiye alimshawishi kuchepuka
naye aliona kitendo cha kumnyima
kingesababisha apoteze ajira yake ambayo
anaitegemea.
Mzee Makelle alipohojiwa, katika hali ya
kustaajabisha baada ya kujitetea alianza
kumchongea Tina kwa mchumbaake akidai si
mwaminifu.


Chondechonde: Babu akiomba msamaha kutoka
kwa makachero wa OFM.

“Wewe kama huyu ni mchumba wako hilo mimi
nilikuwa silijui, lakini huyu mwanamke juzi tu
kalala na mwanaume mwingine palepale gesti na
kama unabisha twendeni nikawaoneshwe kitabu
cha wageni muone jina lake na la huyo bwana,”
alisema mzee huyo.
Waungwana waliokuwa wakimsikiliza mzee
Makelle walimtafadhalisha kutozungumza
maneno ya kichochezi na kumtaka ajitete
mwenyewe.

Baada ya sakata hilo kijana huyo alimchukua
mchumba wake na kuondoka naye ambapo OFM
ilifuatilia na kubaini kuwa bado msichana huyo
anaendelea kufanya kazi kwenye gesti hiyo.
Endapo mfanyakazi huyo atafukuzwa kazi na
bosi wake baada ya kufumaniwa OFM inaiomba
serikali kuingilia kati ili mwanamke huyo apate
haki zake kwani bosi huyo awali alikuwa
akisema huenda katika mchongo wa kumnasa
Tina anahusika.

No comments:

Post a Comment