KHAA! Katika hali ya kushangaza, dada wa kazi
za nyumbani (hausigeli) mkazi wa Tabata jijini
Dar aliyetambulika kwa jina moja la Aneth,
amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kudai
kuwa bosi wake ambaye ni Mzungu
amemlazimisha kufanya mapenzi na mbwa wake.
Mzungu huyo ambaye jina tunalihifadhi, alidaiwa
kufanya tukio hilo la kinyama Mei 26, mwaka huu
na inadaiwa Aneth alipomkatalia, alimtimua
nyumbani hapo kwa kumtupia virago.
Chanzo makini kilidai kuwa, baada ya kutupiwa
virago bila kupewa mshahara wake sambamba
na kipigo, Aneth aliripoti tukio hilo katika Kituo
Kidogo cha Polisi cha Tabata, Dar na muda
mfupi polisi walifika nyumbani hapo lakini
Mzungu huyo hakutoka ndani, akakataa
kuzungumza chochote.
Taarifa zilidai kuwa, baada ya polisi kukutana na
kizingiti hicho, walimpigia simu kiongozi wao
ambaye aliwaamuru warudi kituoni wajipange
upya.
Wananchi wakiwa wamezingira nyumbani kwa
mzungu.
Akisimulia zaidi ishu hiyo, Aneth alisema polisi
walipoondoka eneo hilo, umati uliochukizwa na
kitendo hicho ulikusanyika nje ya nyumba ili
kumdhibiti ‘mtasha’ huyo kwa lolote.
“Kuna jirani mmoja alipiga simu tena kituo cha
polisi alipoona hali ya hewa imechafuka ndipo
polisi wakafika kwa mara nyingine na difenda na
kufanikiwa kuingia ndani kwa kutumia geti
kubwa, walipofika walikuta milango imefungwa
lakini ilisemekana aliruka ukuta na kutimkia
kusikojulikana.
“Polisi waliniambia nimpigie simu ajisalimishe
lakini nilipompigia alisema hayupo na kama
tunamhitaji tukutane sehemu huku na yeye akiwa
na polisi wake,” kilisema chanzo.
Mbwa wa mzungu waliotakiwa kufanya mapenzi
na hausigeli.
Mmiliki wa nyumba hiyo anayeishi Kigamboni,
Mr. Cris alipoulizwa kuhusiana na ishu hiyo,
alikiri kupokea malalamiko na manyanyaso
kutoka kwa Aneth.
Akisimulia zaidi maisha anayoishi na Mzungu
huyo, Aneth alisema: “Alikuwa akinitafutia
sababu za kunitimua kwani hivi karibuni kwa
bahati mbaya nilipoteza ufunguo wa ndani,
akanipiga mateke na kunisababishia maumivu
makali mwilini kiasi cha kushindwa kutembea.
“Lakini lililoniuma zaidi ni hili la kunilazimisha eti
nifanye mapenzi na mbwa wake, amekuwa
akifanya hivyo mara kwa mara mimi nikaona
siyo sawa na nilipokataa ndipo yakanikuta
hayo.”
Aneth aliripoti matukio hayo katika Kituo Kidogo
cha Polisi Tabata na kupewa fomu ya matibabu
(PF-3) sambamba na kufunguliwa jalada la kesi
namba TBT/RB/3132/2014/ SHAMBULIO na
jalada la uchunguzi lenye namba TBT/
IR/1829/2014/UCHUNGUZI.