Tuesday, 27 May 2014

MTUHUMIWA WA MADAWA YA KULEVYA AFIKISHWA MAHAKAMANI.


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu
imemsomea mashtaka raia wa Nigeria, Olabisi
Ibidun Cole (65) ya tuhuma za kukamatwa na
madawa ya kulevya gramu 831.94 zenye
thamani ya shilingi za Kitanzania milioni 37.4.

Mwendesha Mashtaka, Jackson Chidunda,
alisema mbele ya Hakimu Mkazi wa mahakama
hiyo, Frank Mushi, kuwa mshtakiwa
anakabiliwa na tuhuma za kusafirisha dawa za
kulevya alipokamatwa Mei 19, mwaka huu Cole
akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere alipokutwa na madawa aina ya heroin.
Baada ya kusomewa shtaka hilo mshtakiwa
hakutakiwa kujibu lolote kwa kuwa upelelezi
haujakamilika.

Kesi hiyo itasomwa tena katika mahakama hiyo
Juni 10 mwaka huu na mshtakiwa amerudishwa
rumande.
Mtuhumiwa akifikishwa mahakamai.

No comments:

Post a Comment