Mangwea enzi za uhai wake.
Mratibu Mtendaji wa tamasha hilo la ‘Love
Concert –Kumbukumbu ya Mangwea’, Kareeem
Omary ‘KO’ (kushoto) akiwa na familia ya
marehemu Albert Mangwea ‘Ngwair’ Mama
mzazi wa Mangwea (Katikati) na kaka wa
Mangwea, Keneth Mangwea (kulia).
Mratibu Mtendaji wa tamasha hilo la ‘Love
Concert –Kumbukumbu ya Mangwea’, Kareeem
Omary ‘KO’.
Bana ya Love Concert.
Taswira ya Nyumbani kwa Mama Mangwea kwa
sasa.
Na Andrew Chale
MASTAA mbalimbali nchini wakiwemo
wanamuziki wanatarajiwa kushiriki kwenye tukio
maalum la kumbukumbu ya mwaka mmoja tokea
kifo cha marehemu Albert Mangwea ‘Ngwair’ ,
litakalofanyika ndani ya ukumbi wa Nyumbani
Park (Samaki samaki Spot) , Kihonda Morogoro
mjini Juni 28.
Akizungumza na mtando huu , Mratibu Mtendaji
wa tamasha hilo, Kareeem Omary ‘KO’ alisema
maandalizi ya tukio hilo litakalokuwa la kila
mwaka, limepwa jina la ‘Love Concert -
Kumbukumbu ya kifo cha Albert Mangwe’.
Kareem, aliwaomba wadau kujitokeza kwa wingi
kuunga mkono kwenye tukio hilo kwani litakuwa
la kipekee na la aina yake ambalo pia litatoa
fursa kwa wakazi hao pia mikoa jirani na watu
kutoka nje ya Tannzania ambao watauzulia.
“Nawaomba wadau kujitokeza kuonesha
upendo wa pamoja. Kumbukumbu kwa
mpendwa wetu kama ilivyo utamaduni wetu.”
alisema Kareem.
Na kuongeza kuwa, siku hiyo Watu mbalimbali
watapata kupiga picha na mastaa pamoja na
mama mzazi wa Mangwea kama kumbukumbu.
Kareem aliwataja wasanii watakaotoa burundani,
ni pamoja na kutoka kwa kundi la Wanachemba
ambalo pia aliwahi kuwa nalo marehemu
Ngwair, JSqueezer, P Funky Majani na Mswaki.
Kwa upande wa wasanii kutoka Morogoro ni
pamoja na Afande Sele, Team Racers, Mc Koba
Chris wa Marya, Belle 9, Samir, Zombie,
President Mirrow, Jordan wa Dejavu na wengine
wengi.
Katika siku hiyo ya Juni 28, ambayo ndiyo siku
aliyopatwa na umati marehemu, Kareem alisema
kabla ya matukio ya shoo ukumbini, itatanguliwa
na ibada mbili maalum ikiwemo ya Kanisani na
ile ya nyumbani.
Aidha, Kareem alisema katika tukio hilo, ambalo
linatarajia kuanza majira ya jioni ya saa 10 hadi
saa 12 jioni, wametoa fursa kwa watoto kutoa
burudani ikiwemo ya kuimba na nyinginezo na
baadae usiku wa kuanzia saa 2 hadi majogoo
wasanii hao mbalimbali watatawala jukwaa na
burudani ya nguvu ya kumbukumbu.
Marehemu ‘Ngwair’ alifariki dunia akiwa nchini
Afrika kusini, alijizolea umaarufu kwa nyimbo
kama Mikasi na Nisikilize Mi na nyingine nyingi
alizowahi shirikishwa na wasanii mbalimbali
nchini wakiwemo Professa Jay, Nuru, TID, Chidi
Benz na wengine wengi.
No comments:
Post a Comment