Wednesday, 28 May 2014

MASTAA BONGO MOVIE WAONESHA JEURI YA FEDHA.


FEDHA inaongea! Mastaa wanaowakilisha Klabu
ya Bongo Movie Unity na Shirikisho la Filamu
Nchini (TAFF) wameonesha jeuri ya fedha kwa
kuwatunza maharusi, mwigizaji Vanita Omary na
mumewe Paul Mtenda.


Mastaa wa Bongo Movies wakionyesha jeuri ya
fedha katika harusi ya msanii Vanita Omary na
mumewe Paul Mtenda.

Sherehe hiyo ilifanyika Jumamosi iliyopita katika
Ukumbi wa Mwika, Sinza jijini Dar ambapo
pamoja na zawadi nyingine, maharusi hao
waliondoka na shilingi millioni tatu, fedha
taslimu.

Mpango mzima wa kuwamwaga ‘minoti’
uliongozwa na muigizaji Yobnesh Yusuf ‘Batuli’,Mwenyekiti wa Bongo Movie, Steven Mengere
‘Steve Nyerere’, Jacob Steven ‘JB’, Kulwa
Kikumba ‘Dude’ na wengineo ambapo mwishoni
hesabu ya jumla ilitimia shilingi milioni tatu.


Mwenyekiti wa Bongo Movies, Steve Nyerere
akisherehesha katika harusi hiyo.
Kwenye sherehe hiyo, hawakuonesha utengano,
hawakujali kama ni memba wa Bongo Movie au
Shirikisho la Filamu Nchini (TAFF)
lililowakilishwa na rais wake, Simon Mwakifamba
ambaye muda wote alionekana mwenye furaha.

               


Paul Mtenda akiwa na 'mai waifu wake'
Vanitha.

Mbali na Steve Nyerere, JB, Batuli na Dude,
mastaa wengine waliohudhuria sherehe hiyo ni
pamoja na Issa Mussa ’Cloud 112’, Elizabeth
Michael ‘Lulu’, William Mtitu, Single Mtambalike
‘Rich’, Yvonney Cherry ‘Monalisa’, Suzan Lewis
‘Natasha’ na wengine

No comments:

Post a Comment