Msanii maarufu wa Kenya, Nyota Ndogo
amejikuta akimwaga machozi kutokana na aibu
aliyoipata baada ya kundi kubwa la watu
kumshuhudia akiwa uchi wa mnyama huku
akijipaka mafuta pasi yeye kujua.....Nyota Ndogo
alikumbwa na dhahama hiyo alipokuwa aki
perform katika show moja nchini Kenya hivi
karibuni.
"Yani nimekwenda show.nikapewa chumba
chakubadili nguo.nimevua nguo zote najipaka
mafuta pole pole kumbe najiangalia kwa kioo
kumbe upande wapili naoneka kila kitu.yani
nimekosa amani...aibu nilio iona mungu ndio
anajua.sijui wamechukua video..haya ngoja
tusubiri," amendika kwa uchungu msanii huyo
Msanii huyo amemtwisha zigo la lawama
mwenyeji wake aliyempatia chumba hicho ili hali
akijua kinaonekana kwa nje
"Hapana nilibakisha cha ndani na nyonyo ilikua
na nguo pia.kitu sielewi ni alienipeleka kubadili
nguo ina maana hakujua nje naonekana?maana
aliambia kioo hiki jiangalie mpaka
miguu."Ameandika Nyota Ndogo na kuongeza
"Kuajulisha tu ili kama walichukua video
mukiiona mujue niliwataarifu"
Aidha, Nyota Ndogo aliutumia pia ukurasa huo
kuwasihi watu hao wasitoe picha zake za uchi
au video kama walirekodi ili kumtunzia heshima
mbele ya watoto wake
"Wafikirie wanangu," Ameandika
No comments:
Post a Comment