Official fan blog "Classmate" is one among Bongo Classmates properties... It's all about reporting of Current affairs..
Saturday, 17 May 2014
YALIYOJIRI BUNGENI.
Dodoma/Dar es Salaam. Kashfa ya zaidi ya
Sh200 bilioni za Akaunti ya Escrow ya Benki Kuu
ya Tanzania (BoT) imechukua sura mpya baada
ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick
Werema kudai kuwapo kwa watu wanaonunua
mashahidi.
Jaji Werema alitoa kauli hiyo nzito bungeni mjini
Dodoma juzi, kauli ambayo imeibua maswali
mengi kuliko majibu, kuhusu ni nani wanaotoa
fedha kutafuta mashahidi na kwa masilahi ya
nani hasa.
“Ninafahamu kwamba kuna watu wengi
wanatumia fedha kwa ajili ya kutafuta
mashahidi, lakini haituhusu, palipo na haki, haki
itasimama na haki ya mtu haipotei,” alisema
Werema katika kauli inayoonyesha kukata
tamaa.
Werema alitoa wito kwa Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru)
kuendelea na uchunguzi na waufanye haraka na
kwa umakini.
“Uamuzi uliofanyika hapa ni kwamba uchunguzi
uendelee na vyombo vilivyoteuliwa ni Takukuru
na CAG na bado vinafanya uchunguzi… Nahimiza
vyombo hivyo vifanye kazi hiyo haraka na kwa
umakini,” alisema.
Hata hivyo, Werema alitahadharisha kuwa ni
vyema ikafahamika, akaunti ya Escrow
ilianzishwa kwa malengo maalumu. Akaunti hiyo
ilifunguliwa na Kampuni ya IPTL na Shirika la
Umeme Tanzania (Tanesco).
Werema alikiri zipo kodi ikiwamo ya Ongezeko la
Thamani (VAT), ambayo ilipaswa kulipwa na
Tanesco na kodi ya Manufaa (capital gain)
inapaswa kulipwa na Kampuni iliyoiuza IPTL kwa
Pan African Power Ltd (PAP).
Wiki iliyopita, Waziri Mkuu Mizengo Pinda
alisema hoja iliyopo na inayoleta ubishani ni
kuondoa fedha katika akaunti ya Escrow na
kuzipeleka.
Waziri Mkuu alisema: “Kwa tuhuma zenyewe
zilivyo itabidi tuwahusishe Takukuru nao wafanye
kazi kwa upande wao ili kupata ukweli kwa
sababu wako pia viongozi wa Serikali
wanaotuhumiwa katika suala hilo, hivyo ni vyema
likachunguzwa kwa uzito wake ili wale
watakaobainika wamekula rushwa washtakiwe.
Kadhalika Waziri Mkuu aliliomba Bunge
limruhusu CAG kukamilisha kazi hiyo
Labels:
Bunge la Tanzania
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment