Wednesday, 28 May 2014

BINTI ACHANWA KWA VIWEMBE SABABU IKIWA NI WIVU.

Stela Mbinga ambaye ni mke wa mtu, mkazi wa
Tegeta - Kontena jijini Dar amepata balaa kubwa
baada ya kuchanwachanwa uso wake kwa
viwembe na jirani yake aliyefahamika kwa jina la
Zakia Mohamed.



Stella Mbinga akiwa na majeraha ya viwembe.

Habari kutoka eneo la tukio zinasema kuwa,
Zakia na Stella kwa muda mrefu wamekuwa
wakiishi maisha ya uhasama na kuringishiana
hali iliyojenga chuki miongoni mwao.“Hawa huwa
wanashindana kimaisha. Huyu akifanya hivi,
mwingine anafanya vile. Cha kushangaza huwa
wanatishiana hadi mambo ya vyakula, kwamba
nani anakula vizuri zaidi ya mwenzake.
“Sasa juzi Stella alikuwa amekaa kibarazani
wanazungumza na shoga yake, Zakia alipita
akawakuta wanacheka, hata alipokuwa chumbani
wakaendelea na vicheko vyao, akahisi
wanamsema na kumcheka yeye, alipotoka
akamvaa Stella, kumbe alikuwa na kiwembe,
akaanza kumchana bila huruma,” alisema mmoja
wa majirani wa wanawake hao.
Wasamaria wema walimpeleka Stella Kituo cha
Polisi Tegeta ambapo ilifunguliwa kesi nambari
TGT/RB/1969/2014 - Kujeruhi kisha kukimbizwa
katika Hospitali ya Mwananyamala ambako
alishonwa nyuzi 19 usoni na nane kifuani.



Stella akiuguza majeraha.

Akizungumza kwa tabu nyumbani kwake, Stella
alisema: “Amenionea tu, hapa sijisikii vizuri.
Nahisi kizunguzungu na giza kila ninaposimama,
pia siwezi kula vizuri chakula kwani kila
ninapotafuna, kichwa kinaniuma sana.”

No comments:

Post a Comment