Tuesday, 27 May 2014

BIFU LA STEVEN NYERERE NA BATULI LAFIKIA MWISHO.



               Stori: Gladness Mallya


IMEKAA poa sana! Lile bifu lililotia fora kwa
wasanii wa filamu, Steven Mengere ‘Steve
Nyerere’ na Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ huku kila
mmoja akiapa kutopatana na mwenzake,
hatimaye limekwisha siku chache baada ya kifo
cha msanii mwenzao, Adam Philip Kuambiana.
Kwa mujibu wa chanzo makini, wawili hao
walimaliza tofauti zao kutokana na kifo cha
ghafla cha Kuambiana hivyo wakaamua
wenyewe kuyamaliza kwani wameona maisha ni
mafupi.

“Steve na Batuli kwa sasa wameshamaliza
tofauti zao, wamepatana, wanaelewana vizuri
sana na ni baada ya kifo cha Kuambiana ndipo
walikaa wakaamua kuzungumza na kumaliza
tofauti zao,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, Ijumaa
Wikienda liliwasaka wahusika ambapo Batuli
alithibitisha kwamba ni kweli amemaliza tofauti
zake na Steve na sasa wameanza maisha
mapya kwani amegundua maisha ni mafupi na
kifo kinakuja muda wowote.
Kwa upande wa Steve Nyerere alikuwa na haya
ya kusema: “Mimi ndiye Mwenyekiti wa Bongo
Movie Unity na nilishasema nitamaliza tofauti
zote yaani mabifu yote yataisha kwa sababu
mimi ni kiongozi na mfano wa kuigwa
nimemaliza bifu na Batuli naamini na hayo
mengine yataisha, huu ni mwanzo tu.”

No comments:

Post a Comment