Wakati kampuni ya Multichoice Africa ilipokuwa ina-launch moja ya
kampeni yake kubwa inayoitwa glitz and glam content extravaganza nchini
Mauritius, Stage ilimkosa Diamond Platnumz akiwa ndiye anajulikana
kama ndio mwanamuziki maarufu anaye-make headline kwenye upande wa
Afro-pop. Diamond hakuonekana kwa mashabiki waliokua wamefurika
kumshuhudia akifanya vitu vyake, kitendo kilichopelekea mashabiki waanze
kuhuzunika kwa kumkosa Diamond on stage ambayo alibidi afanye show hiyo
pamoja na wakali wengine watano kutoka barani Africa hiyo jana.
Sababu yakukosa kuhudhuria show hiyo, iliyokuwa inasubiriwa na wapenzi
wengi wa muziki huko Mauritius ni kuachwa na ndege, iliyokuwa atoke nayo
kutoka nchini Belgium na kunganisha hadi Mauritius kwenye show hiyo,
hii ni mara nyingine kumtokea Diamond kwa kuachwa na ndege. Diamond
Platnumz hivi sasa inasemekana ndiye msanii kutoka tanzania anayeongoza
kwa kuwa booked mara nyingi kwenye almost kila show kubwa inayofanyika
hapa barani Africa hivi sasa.
No comments:
Post a Comment