Sunday, 1 June 2014

SIMANZI:MAMA ZITTO KABWE AFARIKI DUNIA.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Mama
Mzazi wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini
(Chadema), Zitto Zuberi Kabwe, Bi. Shida wakati
alipokuwa amelazwa ICU katika Hospitali ya AMI
jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Mama mzazi wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini
(Chadema), Zitto Kabwe, Bi. Shida amefariki
dunia akiwa katika Hospitali ya AMI jijini Dar es
Salaam.


Zitto Kabwe kupitia twitter amesema:My mother
has just passed away. Inna lillah wainna illaih
raajiun
Ujumbe wa Zitto

Viongozi na wadau mbalimbali wametuma salamu
za pole kwa Zitto Kabwe.

Bernard Membe
Zitto kabwe pole sana kwako na ndugu kwa
Msiba huu mzito. Tunawaombea subira na
Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahala pema
peponi..Amina

William Ngeleja
Nimepokea Taarifa za msiba wa Bibi Shida Salum
(mama mzazi wa Mhe. Zitto Kabwe) kwa
masikitiko makubwa. Nawapa pole familia nzima
ya ndugu yetu Zitto katika kipindi hiki cha
Majonzi. Mwenyezi Mungu awape Wepesi , na Pia
natoa pole kwa wote walioguswa na Msiba wa
George Otieno aliyefariki Jana. Tuendelee
kuziombea familia hizi na zingine zenye misiba ili
wapate faraja kutoka kwa Mwenyezi Mungu
ambaye ni mfariji Mkuu!

Jokate Mwegelo
Zittokabwe I’m so so sorry Zitto. May her soul
rest in peace. Amen!!

Linex Sunday
Nachukua nafasi hii kuipa pole familia ya Zitto
Ruyagwa Kabwe Ndugu jamaa Marafiki kwa
kumpoteza Bi Shida Mungu awape nguvu katika
kipindi hichi kigumu R.I.P Bi shida tulikupenda
lakini Yeye aliyekuleta amekupenda zaidi Jina LA
Bwana libalikiwe na mapenzi yake yatimie.



CREDIT:BONGO5 .

No comments:

Post a Comment