Friday, 13 June 2014

EXCLUSIVE INTERVIEW:MASOGANGE AKIONGELEA MAISHA YA JELA YA S.A .

Video vixen Agnes Gerald a.k.a Agnes
Masogange amefunguka kuhusu matatizo
aliyoyapata mwaka jana baada ya kukamatwa
uwanja wa ndege wa Or-Tambo, Afrika Kusini
(July 5 2013) na mzigo uliosemekana kuwa ni
dawa za kulevya.

Agnes ni miongoni mwa Watanzania
waliokwenda Durban, Afrika Kusini kumsupport
Diamond Platnumz katika Tuzo za MTV (MAMA)
weekend iliyopita, na Bongo5 ambayo pia
ilihudhuria Tuzo hizo ilipata nafasi ya kufanya
nae Exclusive Interview.
“Ilikuwa ndio mara yangu ya kwanza kuingia
jela sijawahi kuingia jela tangu nizaliwe,
nilivyoingia mle ndani nikawa naomba kila siku
eh Mungu wangu,” alisema Aggy.
Pamoja na mengine, Masogange ambaye kwa
sasa amehamishia makazi yake jijini
Johannesburg, aliweza kushare na sisi jinsi
maisha yake ya jela yalivyokuwa baada ya
kukamatwa na kuwekwa ndani huko Afrika
Kusini. “Nilivyofika pale na watu walivyokuwa
wanachukulia yani na mimi nilikuwa nahisi
labda siwezi kutoka leo wala kesho, nilikuwa
nahisi labda ntapigwa sentence ya miaka kumi
miaka kumi na tano lakini Mungu ni mkubwa
nimetoka.” Alisema.Agnes amesema kuwa kuna
baadhi ya marafiki zake ambao walikuwa
wanatamani afungwe:
“Yah kuna wengine hadi marafiki zangu
walikuwa wanapenda mi nikae ndani, si unajua
sisi yani hatupendani mimi naweza nikakupenda
wewe ukiwa na kitu lakini mimi nikipungukiwa
kitu flani huwezi kuwa rafiki yangu tena sababu
unajua Agnes kakwama kitu flani, kwahiyo
atakuwaje rafiki yangu. Au wengine wanaweza
kuongea ooh Agnes alikuwa anaringa sijui hivi
na hivi bora ameenda jela.”
Alichojifunza Jela:
“Nimejifunza vingi sana sababu kule ndani sio
kuzuri kabisa [kicheko] lakini naona jela ya
huku (South Africa) na Tanzania ziko tofauti,
jela ya huku kidogo unakula vizuri unalala
vizuri baada ya siku mbili mnabadilishiwa
mashuka mnapewa sabuni kila kitu, maji ya
moto mnaoga [kicheko] sijui kama bongo kuna
maji ya moto [kicheko]. Lakini mi nahisi jela ni
jela unajua mtu hata uwe unakaa jela nzuri
ukikosa ule uhuru tu ndio hivyo.’
Masogange pia alizungumzia ukweli wa
kilichotokea hadi kukamatwa na kuwekwa
ndani:
“…Watu walikuwa wanaongea ile ni drugs lakini
sio drugs…, we hujui wanatengenezea nini
mahospitli , zinatumika mahospitali,
zinatengeneza panadol, “
Ushauri kwa wasichana wengine wanaotumiwa
katika biashara ya dawa za kulevya:
Mimi nilikuwa nawashauri yani hizi kazi sio
nzuri ni bora mtu utafute pesa kwa biashara
nyingine lakini sio mambo ya madawa au
kubebeshwa madawa ya kulevya, kwasababu
yani ukishashikwa tu miaka yako ni mingi sana.

No comments:

Post a Comment