Saturday, 7 June 2014

ASHUSHIWA KIPIGO KWA KUZANIWA NI MWIZI.

Kijana mmoja aleyetambulika kwa jina moja la
sule amenusurika kifo baada ya kupingwa na
watu wenye asira kali wakimtuhumu kuwa ni
mwizi jambo ambalo baadae lilikuja kubainika
kuwa hana hatia yoyote.
Wakizungumza eneo la feri jijini dar es salaam
baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamesema
kuwa inasikitisha kuona watu wakijichukulia
sheria mikononi bila kuhoji tukio ambapo mara
baada ya kipigo ambacho kimemsababishia
majeraha makubwa kijana huyo hakuna mtu
aliye jitokeza kulalamika kuibiwa wala
kujulikana kijana huyo ameiba nini.
Akiongea kwa shida kijana huyo amesema kuwa
yeye hakuiba chochote na hajui kwa nini watu
walimvamia na kuanza kumpiga


Katika hatua nyingine ya kujaribu kunusuru
maisha ya kijana huyo baadhi ya wasamalia
wema waliamua kumfikisha kijana huyo katika
vyombo vya usalama lakini mara baada ya
kumfikisha katika kituo kidogo kilichopo karibu
na hapo walikuta kituo hicho kimefungwa na
kufuri na hakuna askali yoyote lakina baada ya
muda askali polisi mmoja alitokea.

No comments:

Post a Comment