Tuesday, 3 June 2014

KUFA KUFAANA:WEMA NA KAJALA YAMEIVA...

Wema Isaac Sepetu na mwigizaji
mwenzake wa sinema za Kibongo, Kajala
Masanja wakiwa pamoja katika hali ya
kupatana.
AMA kweli kufa kufaana! Lile bifu zito
lililokuwa likitokota kati ya wapendwa
wawili, Miss Tanzania 2006/07, Wema
Isaac Sepetu na mwigizaji mwenzake wa
sinema za Kibongo, Kajala Masanja
limekwisha kufuatia kukalishwa katika
kikao cha siri  kilichofanyika kwenye
msiba wa aliyekuwa mwogoza filamu
mahiri nchini, marehemu George Otieno
‘Tyson’, Risasi Mchanganyiko limeinasa.
Kwa mujibu wa chanzo makini,
upatanishi huo ulitokea baada ya wote
wawili kufika kila mmoja kwa wakati
wake kwenye msiba huo nyumbani kwa
marehemu, Makonde, Mbezi-Baech jijini
Dar.
Kabla ya kikao hicho, ‘maadui’ hao kila
mmoja alionesha kuwa kivyake huku
wapambe wakiwaongoza kwenye
‘kambi’ mbalimbali ili wasikutane.
Ilidaiwa kwamba kufuatia hali hiyo,
ndipo baadhi ya mastaa waliamua
kujikusanya na kujadili namna ya
kuwapatanisha wawili hao huku
wakiona kwenye msiba huo ndiyo
mahali mwafaka kwa vile wote wapo.

MUDA WA KIKAO
Chanzo kilidai kwamba, kikao cha
kuwapatanisha Wema na Kajala
kilichukua muda wa saa mbili, kwa
maana ya dakika 120 huku kikifanywa
kuwa siri nzito ambayo haikutakiwa
kufika kwenye vyombo vya habari.
Kajala Masanja
WAJUMBE WA UPATANISHI
Kwa mujibu wa chanzo hicho, wajumbe
wasiopungua nane walishiriki
kuwaweka chini maadui hao na
kusikiliza hoja zao kabla ya
kupatanishwa.
“Kikao kilikuwa kizito kidogo, kilianza
usiku mwingi, lakini kiliisha salama.
“Kajala alionesha ugumu wa kukubali
kupatana kuliko mwenzake (Wema)
lakini wajumbe walikuwa ngangari.
“Wajumbe waliokuwepo ambao wote ni
watu wa filamu ni Single Mtambalike
‘Richie’, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’,
Hartmann Mbilinyi, Vincent Kigosi
‘Ray’, John Lista na mwingine
alliyetambulika kwa jina moja la
Lamatha,” kilisema chanzo chetu kwa
kujiamini.

BAADA YA USULUHISHI
Chanzo kilisema kuwa baada ya
kumaliza upatanishi huo, wawili hao
walibaki wenyewe ambapo waliongea
mambo mbalimbali kuhusu maisha kwa
sasa.
“Kusema ule ukweli hawa watu
wamepatana kweli, wala si sinema.
Hata baada ya usuluhishi, waliachwa
wenyewe ambapo walizungumza
mambo yao,” kilisema chanzo hicho.
Wema Isaac Sepetukatika pozi tofauti.

HISTORIA YA BIFU
Machi 25, 2013, Kajala alihukumiwa
kwenda jela miaka mitano kufuatia kesi
yake ya kuuza nyumba iliyowekewa
zuio halali na Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa nchini
(Takukuru).
Kesi hiyo ilihukumiwa katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
jijini Dar ambapo Wema alimlipia
Kajala faini ya shilingi milioni 13 na
kumfanya mshitakiwa huyo kuwa huru.
Baada ya hapo, wawili hao wakawa
marafiki wakubwa huku Kajala
akifanya kazi ya ukatibu kwenye ofisi
ya Wema ya Endless Fame Production,
Mwananyamala jijini Dar (kabla
haijafungwa).

BIFU
Haikujulikana mara moja nini kilitokea,
lakini ghafla wawili hao wakawa
maadui. Madai ya chanzo yalisema bifu
lao lilitokana na kitendo cha Kajala
kumchukua ‘bwana’ wa mwenzake
anayejulikana kwa jina la CK au kigogo
wa ikulu.
Huyo kigogo wa ikulu, awali alikuwa
mpenzi wa Wema na Kajala kuwa
shemeji yake ‘automatiki’.
Chanzo kingine kilisema bifu lao
lilitokana na kitendo cha Wema
kuhamishia ushoga kwa staa mwingine
wa filamu, Aunt Ezekiel hivyo
kumfanya Kajala kuwa ‘wazamani’.

UKWELI WA BIFU
Hata hivyo, ukweli wa kuwepo kwa bifu
lao ulijitokeza siku moja Kinondoni
jijini Dar ambapo Wema alikuwa saluni,
Kajala naye akafika, Wema alitoka ili
kumkumbatia lakini Kajala akamkwepa
na kumwambia atamchafua.
Inadaiwa Wema alikasirika na
kumtukana Kajala hali iliyokoleza bifu
lao ambalo awali lilikuwa chini kwa
chini. Ilidaiwa siku hiyo Wema aliamua
kutumia nafasi hiyo ya kukumbatiana
ili kuondoa minong’ono ya siku nyingi
kwamba wana bifu.
Hata hivyo, katika mahojiano maalum
na mwandishi wetu, Wema alikiri
kuhusu Kajala kumkwepa lakini
akaongeza kuwa, bifu lao liliungwa
mchuzi kufuatia kitendo cha Kajala
kumsema vibaya kuhusu fedha zake.
Wema alisema kuna wakati walikwenda
Arusha kwenye shoo iliyoandaliwa na
kampuni yake, yeye akawa na uhutaji
wa fedha ambapo alimuomba Kajala.
Alisema licha ya kumkopesha ikiwa
imepungua kidogo, lakini Kajala
alimwita mdogo wake mmoja na kumpa
fedha nyingine akimwelekeza
akaziweke benki kwa vile anahisi Wema
atazimaliza.

SHUTUMA HADHARANI
Kuanzia hapo, Wema na Kajala
walikuwa wakiropokeana kwenye
vyombo vya habari. Kuna siku Wema
alidiriki kutoa tamko kwamba, kwa hali
ilivyo anajuta hata kumtolea zile
shilingi milioni 13. Akasema angejua
angemwacha akafungwe jela.
Habari hiyo iliandikwa na Gazeti la
Ijumaa la Aprili 25, mwaka huu ikiwa
na habari yenye kichwa; NAJUTA
KUMLIPIA KAJALA MIL. 13!

WADAU WASHUKURU
Tukirudi kwenye chanzo, kilisema
wadau waliosikia kupatana kwa wawili
hao ndani ya msiba wa Tyson
walishukuru wakiwaombea kwa Mungu
awape uzima.

KUHUSU MWILI WA TYSON
Kwa upande mwingine, mwili wa
George Tyson uliagwa jana kwenye
Viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini
Dar na kusafirishwa kwa ndege kwenda
nchini Kenya kwa mazishi.

No comments:

Post a Comment