Saturday, 7 June 2014

BREAKING NEWS:KUHUSU KIFO CHA MZEE SMALL.(MUIGIZAJI MKONGWE TANZANIA).



Muigizaji mkongwe aliyetamba miaka
mingi kwa filamu za vichekesho Said
Ngamba maarufu kwa jina la Mzee Small
amefariki dunia usiku wa kuamkia leo
katika hospitali ya taifa ya Muhimbili.



Habari hizi za kusikitisha zimeripotiwa
na chanzo cha kuaminika ambacho
kimeeleza kuwa alizidiwa na ugonjwa wa
presha uliopelekea kifo chake.

Muigizaji huyo amekuwa akisumbuliwa
na magonjwa kwa muda mrefu hali
iliyompelekea kulemaa viungo hususani
mkono wake.

Taarifa hizi ni mwiba mwingine kwa
tasnia ya filamu nchini ikiwa ni wiki moja
imepita tangu marehemu George Tyson
afariki kwa ajali ya gari.

Mungu ailaze pema roho ya Mzee Small.
Amina!


CREDIT:SAM MISAGO.

No comments:

Post a Comment