baada ya miaka minne, hapa ndipo diamond na wema walipoamua kufikia.
Ni miaka minne imepita hadi sasa toka mahusiano yao yalipoanza, unaweza
kusema kati ya vitu ambavyo wamepitia wawili hawa(Wema na Diamond ), ni
misukosuko ya hapa na pale, moja ya vitu ambavyo vimeweza kuweka
mahusiano yao yasimame imara hadi hivi sasa. Safari ya miaka minne mbali
na kuwa na vikwazo vingi, ikiwemo kuachana na kurudiana mara kwamara,
kuumizana wenyewe kwa wenyewe katika safari yao, Wema Sepetu alitokea
kufunguka kuwa hivi sasa inatosha, na haina budi kutulia.
Wapenzi hao maarufu sana, ikiwa ni moja ya celebrity couple yenye nguvu
zaidi, ikiwa kila mmoja wao ana fanbase kubwa sana(mashabiki), walitokea
kufunguka mapema mwaka huu kfikia kwenye uamuzi wa kukaa chini na
kupanga mipango makini sana ya kuwa mume na mke, hii ni moja ya hatua
ambayo si watu wengi, au wasani wengi wameweza kufikia hadi hii leo,
mbali na watu wengine kutabiri kuwa, mapenzi yao hayatadumu, ila vitendo
vyao na malengo yao katika kujipanga hivi sasa inaonyesha kuwa watabiri
hao wataendelea kusubiri sana.
Wema alitokea kusema kuwa bila nguvu ya mashabiki wake ambao anawapenda
sana, hii leo yeye na Diamond Platnumz wasingekuwa hapa sehemu hii
walipo katika maisha ya mahusiano yake, Wema sepetu alizidi kufunguka na
kusema kuwa inakuwa inatia moyo kwa shabiki mtu ambaye hata hujawahi
kukutana nae anaweza kuonyesha mapenzi makubwa kwake, na kuweza kuwa
katika sehemu kubwa ya maisha yake, hii ni kutokana na mara nyingi
ugomvi wowote utokeapo kwenye mitandao, mashabiki wake ndio wanamalizaga
na kutuliza ugomvi huo, hadi kufikia kipindi wema kusemekana kuwa huwa
anawatuma mashabiki wake, jambo ambalo si kweli bali ni mapenzi yao
kwake kwani wako teyari kupigana kwa ajili yake.
No comments:
Post a Comment