HUKU akiacha wake watatu, Yvonne-Sheryl
Ngatikwa ‘Monalisa’, Beatrice na Lucy, msiba wa
marehemu George Otieno ‘Tyson’ (41) umezua
maajabu kwa kuwa na majeneza mawili, Uwazi
linakumegea moja moja.
Kwenye gari ni moja ya jeneza lilikusudiwa
awali kutumika kwa ajili ya kuuhifadhi mwili wa
marehemu George Otieno,' Tyson'.
Kwa mujibu wa chanzo, uwepo wa majeneza
hayo ulitokana na kukosekana kwa usimamizi
imara kiasi cha kuyafanya yakosolewe kwa
kukosa ubora kulingana na hadhi ya marehemu
na hivyo nusura linunuliwe la tatu.
Msanii wa Bongo Fleva, Ambwene Yesaya ‘AY’
akijitolea shilingi laki sita kufanikisha ununuzi
wa jeneza la pili.
JENEZA LA KWANZA
Jeneza la kwanza lilikuwa la mbao bila ishara
kwamba ni jeneza. Wengi waliliita sanduku
kutokana na muundo wake na lilifikishwa
hospitali tayari kwa kuubeba mwili wa
marehemu.
JENEZA LA PILI
Msanii wa Bongo Fleva, Ambwene Yesaya ‘AY’
alipofika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro
alishtushwa kuwepo kwa jeneza hilo hivyo
alijitolea kwenda kununua jingine kwa gharama
ya shilingi 600,000.
Jeneza la pili likichukuliwa tayari kwa
kuuhifadhi mwili wa marehemu Tyson.
MCHANGO MKUBWA
Akizungumza na Uwazi juzi, Rais wa Shirikisho
la Filamu Tanzania ‘Taff’, Simon Mwakifwamba
alikiri kuwepo kwa majeneza mawili lakini
akasema AY aliokoa jahazi kwa kununua la pili
lenye ubora.
Hata hivyo, baada ya jeneza la pili kuufikisha
mwili kwenye Hospitali ya Kairuki jijini Dar,
wasanii wa Bongo Movie walilipinga wakidai nalo
pia halikuwa na hadhi ya kubebea mwili wa
Tyson hadi Kisumo, Kenya ambako marehemu
atazikwa.
“Lile jeneza alilonunua AY nalo si bora sana
ukilinganisha na majeneza ya marehemu Adam
Kuambiana na Recho Haule. Tyson si mtu wa
kumweka kwenye jeneza kama hili. Tutatafuta
jingine lakini tutamwambia AY atusamehe,”
alisema Katibu wa Bongo Movie, William Mtitu.
Marehemu George Otieno,' Tyson' enzi za uhai
wake.
Naye Mwakifwamba akizungumzia kuhusu
kununua jeneza jingine na kuachana na lile
lililosafirishia mwili kutoka Morogoro, alisema:
“Kikao cha mwisho tumekubaliana kwamba,
jeneza litumike lilelile la Morogoro ila lifanyiwe
decoration (mapambo) ili liweze kuwa la kisasa
zaidi.”
MKUU WA WILAYA
Mwakifwamba alikwenda mbele zaidi kwa
kusema, AY mbali na kununua jeneza lakini pia
alinunua shati jipya la marehemu kufuatia T-shirt
aliyoivaa siku ya ajali kujaa damu.
Akaongeza: “Wa kuwashukuru ni wengi, mfano
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka
yeye ndiye aliyetoa usafiri wa gari (Toyota Land
Cruiser) kwa ajili ya kuleta mwili wa marehemu
hapa Dar.”
MWILI KUSAFIRISHWA KENYA
Naye ndugu wa marehemu Tyson, Felix Owino
alipozungumza na Uwazi juzi alisema kikao cha
familia kimeamua kuusafirisha mwili kwenda
kuzikwa Kisumo, Kenya.
Alisema mwili utasafirishwa Jumanne (leo) au
Jumatano kulingana na kukamilika kwa bajeti
ambayo ni shilingi milioni 19. Aliongeza kuwa,
mwili huo utaagwa kwenye Viwanja vya Leaders
Club, jijini Dar es Salaam.
Marehemu Tyson alifariki dunia kwa ajali ya gari
aina ya Toyota Noah, Ijumaa iliyopita wakati
yeye na wenzake wakitokea Dodoma kwenda
Dar. Wengine watatu walijeruhiwa na wanatibiwa
katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, akiwemo MC
maarufu, Gladness Chiduo ‘Zipompa’.
Ajali hiyo ilitokea maeneo ya Gairo kuelekea
Morogoro. Marehemu ameacha watoto wawili.
No comments:
Post a Comment