Saturday, 7 June 2014

ACHOMWA BISIBISI NA MUMEWE BAADA YA KUMFUMANIA NA HOUSEGIRL.

Tofauti na inavyoaminika na wengi kuwa
mfumaniwaji huwa mpole, kibao kimebadilika,
mfanyakazi wa ndani aliyejulikana kwa jina la
Niachie amegeuka mbogo na kumchoma bisibisi
bosi wake, Amina ‘Mama Zai’ aliyemfumania
akiwa na mumewe aitwaye Amri.
         
Amina au Mama Zai akionyesha jeraha
alilojeruhiwa na mfanyakazi wake wa ndani
baada ya kumfumania akiwa na mumewe.
Tukio hilo lilitokea juzikati maeneo ya Mbagala
jijini Dar ambako mama Zai alimwekea mtego
mfanyakazi wake huyo wa ndani baada ya
kubaini kuwa alikuwa akitembea na mumewe
wakati yeye akiwa kazini.
ISHU ILIVYOANZA
Akizungumza na paparazi wa kitengo maalum
cha kufichua maovu (OFM) siku mbili kabla ya
tukio, mama Zai alidai kuwa mumewe ana
kawaida ya kufanya mapenzi na mfanyakazi wao
wa ndani wakati yeye akiwa kazini hivyo
akaandaa mtego ili kukomesha tabia hiyo.

                   
Chumba walichonaswa mume na hausigeli.
KUMBE NI NESI
Mama Zai alizidi kumwaga data kuwa, yeye ni
nesi katika hospitali moja ya mtu binafsi iliyoko
Jangwani jijini Dar hivyo akiwa zamu ya usiku,
mumewe hutumia mwanya huo kubanjuka na
hausigeli.
“Ananivizia nikitoka tu na akijua nimeshafika
mbali, anaingia chumbani kwa hausigeli na
kuvunja naye amri ya sita,” alidai mama huyo.
MTEGO WANASA
Mama huyo alisema ili kufanikisha zoezi la
kumnasa mumewe, alijifanya anakwenda zamu
ya usiku kisha akajifungia stoo ili aweze kufanya
fumanizi matata.
Kama kawa, OFM ilitia timu nyumbani kwa
mama huyo ikiwa kamili na zana zake, ikakita
kambi katika baa moja iliyo jirani na nyumba
hiyo na ilipofika saa tano usiku, ishu ikatiki,
baba Zai aliingia katika chumba cha mfanyakazi
huyo kwa lengo la ‘kuharibu’.

         

                'MISS IN ACTION’
Wakati makamanda wa OFM wakiwa ‘wanaseti’
kamera zao huku wakisubiri polisi na mwenyekiti
wa serikali za mtaa wafike eneo hilo, mama Zai
alivamia chumba hicho (alihofia baba atamaliza
mchezo) na purukushani ya nguvu ikaanza.
Katika harakati za kujinasua katika kipigo cha
bosi wake, hausigeli huyo aliokota bisibisi na
kumchoma mama mwenye nyumba shingoni
kisha kutimua mbio huku mume naye akiingia
mitini.

No comments:

Post a Comment