Saturday, 7 June 2014

WATESAJI WATOTO WAKIONA CHA MOTO.....PICHAZ

Jeshi la Polisi Changombe, Dar linamshikilia
mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Neema
na babu Ramadhan kwa RB namba CHA/
RB/4645/2014 UNYANYASAJI WA MTOTO
wakidaiwa kumsulubu mjukuu wao (jina
linahifadhiwa kimaadili).


Mke na mume wanaodaiwa kumfanyia ukatili
mtoto huyo

Tukio la kuwatia nguvuni wahusika hao lilijiri
Mei 29, mwaka huu maeneo ya Buza jijini Dar,
baada ya ya majirani kusikia kilio cha mtoto
huyo akiomba msaada ili kunusuru maisha yake
kutokana na kipigo kizito alichodaiwa kupewa
na wawili hao.
MAJIRANI WAZINGIRA
Kwa mujibu wa majirani waliozingira nyumbani
hao, siyo mara ya kwanza kwa mtoto huyo
ambaye ni yatima kupigwa hivyo waliamua
kuivamia nyumba hiyo kwa kuwataka wazee hao
waache kumpiga mtoto huyo jambo ambalo
lilishindikana.


Mtoto akionyesha majeraha baada ya kipigo

Majirani hao waliokerwa na kitendo hicho
walitishia kuchoma moto nyumba hiyo ndipo
wazee hao wakaacha kumpiga mtoto huyo na
kutoka nje wakijitetea kuwa walikuwa
wakimpiga kwa kuwa alifanya kosa.
Walipohojiwa sababu za kumpiga mtoto huyo
mara kwa mara, wazee hao walijitetea kuwa
mtoto huyo ni mtukutu.


Moja ya majeraha aliyosababishiwa baada ya
kipigo

Majirani hao walidai kuwa siku za nyuma wazee
hao walishawahi kuandamana kuhusu
unyanyasaji wa mtoto huyo ambapo walishawahi
kumripoti polisi Chang’ombe.
MAJIRANI WAANDAMANA
Ilielezwa kuwa majirani hao waliripoti kuhusu
unyanyasaji huo kwa Mjumbe na Afisa Mtendaji
wa eneo hilo, Mary Patrick ambaye alitoa
taarifa kwa mwanaharakati wa kutetea haki za
watoto kutoka TUHIMIZANE, Cleophace Simioni
ambaye alimchukua mtoto huyo na kumpa
huduma ya kwanza kabla ya kumpeleka Ustawi
wa Jamii kwa ajili ya matunzo.


WAANDISHI WASHUHUDIA
Waandishi wetu walifika nyumbani hapo na
kushuhudia mtoto huyo akiwa na majeraha ya
kuchanwa mgongoni, makovu ya moto na
uvimbe usoni na kichwani.
Akizungumzia sakata hilo, mwanaharakati huyo
alisema atapambana hadi hatua ya mwisho
kutetea haki ya mtoto huyo.


Naye Afisa Mtendaji wa Kata ya Buza, alisema
kuwa anapinga vikali unyanyasaji wa watoto
katika eneo lake na kuapa kufuatilia kwa
upande wake ili kuhakikisha wanatoa mfano
kwa watu hao.
Mwishowe wazee hao walifikishwa katika kituo
cha polisi Chang’ombe ambapo walifunguliwa
shitaka hilo wakisubiri kufikishwa kwenye
vyombo vya sheria.

No comments:

Post a Comment