Sunday, 9 November 2014

TAARIFA YA KIFO CHA MUIMBAJI WA TWANGA PEPETA.



Mwimbaji wa zamani kutoka Bendi ya
African Stars ‘Twanga Pepeta’ Khamis
Kayumbu maarufu kama ‘Amigolas’
amefariki dunia usiku wa kuamkia leo
kwenye hospital ya taifa muhimbili
alikokuwa akitibiwa.

Amigo alilazwa Muhimbili kwa
matatizo ya moyo ambapo kwa sasa
msiba uko nyumbani kwa mama
mzazi wa marehemu Mburahati Dar
es Salaam jirani na Shule ya Msingi
Mianzini na taratibu za mazishi
zinasubiri ndugu na jamaa kutoka
Tabora na Kigoma.



CREDIT:MILLARDAYO.COM

No comments:

Post a Comment