[image_0]
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mheshimiwa
Jakaya Mrisho Kikwete alfajiri
ya jana, Jumamosi, Novemba 8,
2014, alifanyiwa upasuaji wa
tezi dume (prostrate) katika
Hospitali ya Johns Hopkins
iliyoko Baltimore, Jimbo la
Maryland, Marekani.
Rais Kikwete amefanyiwa
upasuaji huo baada ya
madaktari waliomfanyia
uchunguzi wa afya yake
kujiridhisha kuwa Rais
alikuwa anahitaji matibabu ya
aina hiyo.
Upasuaji huo uliofanyika
alfajiri na kuchukua kiasi cha
saa moja unusu, umefanyika
salama na kwa mafanikio
makubwa.
Hali ya Mheshimiwa Rais
Kikwete inaendelea vizuri,
bado yuko wodini akiendelea
kuwa chini ya uangalizi wa
madaktari na kupatiwa tiba.
Wananchi wataendelea
kupewa taarifa sahihi kuhusu
hali ya Rais Kikwete kwa kadri
zitakavyokuwa zinapatikana.
Imetolewa na
KURUGENZI YA MAWASILIANO
YA RAIS,
IKULU DAR ES SALAAM,
NOVEMBA 9, 2014
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania,Mheshimiwa Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete
akizungumza na Dkt.Edward
Shaeffer wa hospitali ya Johns
Hopkins (kushoto) na Daktari
wa Rais Profesa Mohamed
Janabi (kulia) muda mfupi
baada ya kuwasili ili
kufanyiwa upasuaji katika
Hospitali ya Johns Hopkins
iliyopo Baltimore Maryland
Marekani Jumamosi
asubuhi.Upasuaji huo
uliochukua muda wa saa moja
na nusu ulifanyika salama.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho
Kikwete akizungumza na
daktari Bingwa Mpasuaji
Edward Shaeffer muda mfupi
kabla ya kuingia kwenye
chumba cha upasuaji
uliofanyika katika Hospitali ya
Johns Hopkins iliyopo Baltimore
Maryland nchini Marekani
Jumamosi asubuhi(picha na
Freddy Maro)
[image_1]
CREDIT:MICHUZI BLOG
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mheshimiwa
Jakaya Mrisho Kikwete alfajiri
ya jana, Jumamosi, Novemba 8,
2014, alifanyiwa upasuaji wa
tezi dume (prostrate) katika
Hospitali ya Johns Hopkins
iliyoko Baltimore, Jimbo la
Maryland, Marekani.
Rais Kikwete amefanyiwa
upasuaji huo baada ya
madaktari waliomfanyia
uchunguzi wa afya yake
kujiridhisha kuwa Rais
alikuwa anahitaji matibabu ya
aina hiyo.
Upasuaji huo uliofanyika
alfajiri na kuchukua kiasi cha
saa moja unusu, umefanyika
salama na kwa mafanikio
makubwa.
Hali ya Mheshimiwa Rais
Kikwete inaendelea vizuri,
bado yuko wodini akiendelea
kuwa chini ya uangalizi wa
madaktari na kupatiwa tiba.
Wananchi wataendelea
kupewa taarifa sahihi kuhusu
hali ya Rais Kikwete kwa kadri
zitakavyokuwa zinapatikana.
Imetolewa na
KURUGENZI YA MAWASILIANO
YA RAIS,
IKULU DAR ES SALAAM,
NOVEMBA 9, 2014
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania,Mheshimiwa Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete
akizungumza na Dkt.Edward
Shaeffer wa hospitali ya Johns
Hopkins (kushoto) na Daktari
wa Rais Profesa Mohamed
Janabi (kulia) muda mfupi
baada ya kuwasili ili
kufanyiwa upasuaji katika
Hospitali ya Johns Hopkins
iliyopo Baltimore Maryland
Marekani Jumamosi
asubuhi.Upasuaji huo
uliochukua muda wa saa moja
na nusu ulifanyika salama.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho
Kikwete akizungumza na
daktari Bingwa Mpasuaji
Edward Shaeffer muda mfupi
kabla ya kuingia kwenye
chumba cha upasuaji
uliofanyika katika Hospitali ya
Johns Hopkins iliyopo Baltimore
Maryland nchini Marekani
Jumamosi asubuhi(picha na
Freddy Maro)
[image_1]
CREDIT:MICHUZI BLOG
No comments:
Post a Comment