Wednesday, 12 November 2014

BAADA YA KUMALIZA TOFAUTI ZAO,WEMA NA PENNY WAINGIA MZIGONI.




Baada ya staa wa filamu
Wema Sepetu na mtangazaji
wa radio VJ Penny weekend
iliyopita kumaliza tofauti zao
zilizowatenganisha kwa
muda mrefu, hatimaye sasa
wameanza kuwa karibu.

Kupatanishwa kwao
kulikofanywa na rafiki yao
Junaithar aliyewaalika
kwenye dinner ya birthday
yake usiku wa Jumamosi,
haukuishia hapo bali sasa
wamerudisha ukaribu kiasi
cha kuanza kutembeleana.

Kupitia Instagram Wema
ameshare picha hii mpya
akiwa na Penny nyumbani
kwake na kuandika:

“And the Saga continues… I
must say I am a Happy
Soul…. So at peace….
Kajisemea shem lake na
nanukuu ” kwenye vitu flani
vya PROJECT…..”
@vjpenny04 @jumalokole2 ″

Penny naye alii-repost.

Lakini ukaribu wao wa sasa
unaonekana pia unahusisha
kazi, kupitia akaunti ya mtu
ambaye Wema amemtag
kwenye picha hiyo

@jumalokole2, naye alipost
picha hizo alizopiga nao, na
kuandika caption
zinazoashiria walikuwa
wanarekodi kipindi.
jumalokole2: “Watu makini
tukifanya yetu new Project
@wemasepetu
@vjpenny04…..” na nyingine
aliandika “Kwenye vitu flani
vya PROJECT…..! “

No comments:

Post a Comment