YEMI: NAKUJA KUMTEKETEZA SHILOLE
MKALI wa
muziki kutoka pande za Nigeria, Yemi Alade amesema yupo tayari kuja
kumteketeza mkali wa miondoko ya mduara Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’
katika Tamasha la Usiku wa Matumaini litakalofanyika Agosti 8, katika
Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Akizungumza na Over The Weekend, kwa njia ya simu, Yemi ambaye ametokea
kujizolea umaarufu mkubwa kupitia wimbo wa Johnny, alisema kuwa
amejipanga vya kutosha na haoni kama kuna mwanamuziki atakayemsumbua
hapa Bongo huku akisisitiza anakuja kumteketeza Shilole ambaye aliambiwa
kuwa anatisha Bongo.
“Tanzania ni nchi nzuri najua na wanamuziki wake wapo vizuri, nimeambiwa
kuna mwanamuziki anaitwa Shilole mwambieni tu nakuja kumteketeza na
shoo zangu huwa hazina mpinzani.
“Nitafanya shoo ya mwaka ya kihistoria siku hiyo na lazima nimchukue Johnny wangu uwanjani hapo na kurudi naye kwetu Nigeria,” alisema Yemi.
“Nitafanya shoo ya mwaka ya kihistoria siku hiyo na lazima nimchukue Johnny wangu uwanjani hapo na kurudi naye kwetu Nigeria,” alisema Yemi.
Yemi anatarajiwa kushuka Dar kesho Jumanne saa tano kamili usiku na
Shirika la Ndege la Kenya Airways, tayari kwa kupiga shoo ya kufa mtu
ambapo ataungana na wakali kutoka Bongo kama Ali Kiba, Shilole, R.O.M.A,
Meninah, Navy Kenzo, Nyandu Toz, P-Plan, Juma Nature na kundi zima la
TMK Wanaume Halisi pamoja na Rais wa Manzese, Madee.
Pia kutakuwa na burudani tofauti katika tamasha hilo ambazo ni ndondi,
mechi kali kati ya timu ya Azam FC dhidi ya Mtibwa Sugar FC, Wabunge
Mashabiki wa Simba dhidi ya Yanga, Bongo Fleva dhidi ya Bongo Movie na
Wanamuziki wa Injili.
No comments:
Post a Comment