AUNT, NICE CHANDE WATIFUANA KWA MITUSI!
STAA wa filamu Bongo,
Aunt Ezekiel na shostito wake Nice Chande, juzikati walijikuta
walitifuana kwa matusi makali ya nguoni nyumbani kwa rafiki yao Wema
Sepetu ‘Madam’ anayeishi mtaa wa Bwawani, Kijitonyama jijini Dar es
Salaam.
Chanzo makini cha habari kilichokuwa nyumbani kwa Wema, kililidokeza
gazeti hili kuwa waigizaji hao wakiwa na rafiki yao mwingine, walianza
kutukanana kwa jambo ambalo halikuweza kubainika mara moja, huku Madam
akijitahidi kuwasuluhisha bila mafanikio.
Wakiwa na dalili zote za kubugia kiburudisho cha kutosha kilichowafanya
wasione vibaya kupaza sauti za matusi mbele za watu, marafiki hao
walitoka ndani ya nyumba hiyo na kuendelea kutukanana kana kwamba hawana
akili nzuri.
Baada ya kuona watu wameanza kukusanyika usiku huo ili kushuhudia sinema
hiyo, Aunt, Nice na rafiki yao walijipakiza kwenye gari, huku Aunt
akiwa nyuma ya usukani na kuanza safari kwa ajili ya kuelekea nyumbani
kwake, Mwananyamala, lakini safari yao iliishia hatua chache mbele baada
ya dereva huyo kulitumbukiza mtaroni gari hilo.
Kuona hivyo, watatu hao walishuka na kuanza kurudi tena nyumbani kwa
Wema, ambaye aliendelea kuwasihi lakini wakiendelea kushambulia kwa
maneno makali, kila mmoja akimlaumu mwenzake kuwa ndiye chanzo cha ajali
ile.
Nyumbani kwa Wema, wasanii hao walimuomba msaidizi wake, Petit Man aende
kuwasaidia kulinasua gari hilo mtaroni, kazi ambayo ilifanywa na vijana
wa mtaani hapo waliolipwa kiasi cha shilingi 50,000.
Hata hivyo, baada ya gari hili kuletwa kwa Wema, si Aunt wala Nice waliokuwa tayari kulipanda, hali iliyomlazimisha mwenyeji wao kupiga simu kuita teksi, ambayo pia baada ya kufika, Nice alikataa kuipanda, badala yake Aunt na shostito wao mwingine ndiyo waliingia ndani na kutokomea.
Baada ya kukubaliana kuwa gari lile lilale hapo, Wema alimtaka Nice
kuingia ndani, lakini aligoma, akidai anataka kuongea na baby wake kwa
njia ya simu, lakini mwenyeji wake aliamua kuita teksi nyingine ambayo
ilifika na kumchukua.
Hata hivyo, baada ya gari hili kuletwa kwa Wema, si Aunt wala Nice waliokuwa tayari kulipanda, hali iliyomlazimisha mwenyeji wao kupiga simu kuita teksi, ambayo pia baada ya kufika, Nice alikataa kuipanda, badala yake Aunt na shostito wao mwingine ndiyo waliingia ndani na kutokomea.
No comments:
Post a Comment