Sunday, 31 August 2014

Pichaz za Feza Kessy, Shaa, Maua na Recho walivyotokelezea kwenye Fiesta ya Moshi.


Home » Ent. » Pichaz za Feza Kessy, Shaa, Maua na Recho walivyotokelezea kwenye Fiesta ya Moshi.

Pichaz za Feza Kessy, Shaa, Maua na Recho walivyotokelezea kwenye Fiesta ya Moshi.

4Feza Kessy ni miongoni mwa Wasanii waliokua wanasubiriwa kwenye stage ya Serengeti Fiesta 2014 hapa Moshi show iliyofanyika August 30 ambapo staa huyu alieiwakilisha Tanzania kwenye BBA 2013, alipanda kwenye stage na dancers wake watatu wa kiume.
Waimbaji wengine wa kike waliochukua mic kwenye stage ni pamoja na Shaa, Maua na Recho.
5
6
35
Shaa kazini
34
33
32
31
30
29
8
Maua
7
16
Recho
17
18
19
Tags :

Shinji Kagawa ameondoka Man United – hii ndio timu aliyoenda


Home » General News » Shinji Kagawa ameondoka Man United – hii ndio timu aliyoenda

Shinji Kagawa ameondoka Man United – hii ndio timu aliyoenda

IMG_6898.JPG
Yamebaki masaa takribani 30 kabla ya dirisha la usajili kufungwa, taarifa mpya ni kwamba kiungo wa kimataifa wa Japan na Manchester United Shinji Kagawa ameihama klabu hiyo.
Kagawa aliyejiunga na Man United misimu miwili iliyopita amerudi kwenye klabu aliyotoka ya Borrusia Dortmund ya Ujerumani.
Man United walimnunua Shinji kwa ada ya uhamisho wa £12m na leo hii imethibitishwa kwamba amejiunga na Dortmund kwa £8m.
Wakati huo huo mwanasoka wa Uholanzi aliyekuwa anakipiga kwenye klabu ya Ajax Daley Blind amefanyiwa vipimo vya afya tayari kujiunga na Man United kwa ada ya £13m.

#Exclusive: Mambo 6 ya kufahamu kuhusu Linah na hit single ya ‘Ole Themba’


Home » Ent. » #Exclusive: Mambo 6 ya kufahamu kuhusu Linah na hit single ya ‘Ole Themba’

#Exclusive: Mambo 6 ya kufahamu kuhusu Linah na hit single ya ‘Ole Themba’

Screen Shot 2014-09-01 at 1.49.10 AMNafasi yake nyingine kubwa ya kuzungumziwa toka ameanza muziki ni hii aliyoipata baada ya kufanya wimbo wa ‘Ole Themba’ na kundi maarufu la Uhuru South Africa.
Ni kolabo ambayo mpaka August 31 2014 usiku video yake YouTube ilikua imebakiza sio chini ya views elfu mbili ili kufikisha views laki moja za wote walioitazama toka iweke July 2014.
Yafuatayo ni mambo 6 ya kufahamu kuhusu Linah na hit single ya ‘Ole Themba’.
1. Video hii ya ‘Ole Themba’ imeanza kuchezwa kwenye vituo vikubwa vya TV Africa ikiwemo MTV Base pamoja na TV ya Ufaransa ya TRACE Urban ambao tayari wameshamtumia Linah mkataba wa makubaliano.
2. Wakati aliposafiri kwenda Afrika Kusini kuirekodi hii single na Uhuru, alikaa kwa mwezi mmoja bila kufanya chochote mpaka kufikia kukata tamaa manake Uhuru kama walimuwekea ‘pozi’ japokua Linah alikua na pesa mkononi tena milioni za Tanzania kwa ajili ya kulipia kurekodi nao hiyo single kama makubaliano yalivyokuwa.
3. Linah anasema Producer wa Uhuru aliwatajia hela nyingi kurekodi hiyo kolabo akidhani watashindwa kuilipia lakini haikua hivyo, mwanzoni aliwawekea pozi kwa kuagiza atumiwe link za video za Linah YouTube ili ajue uwezo wake lakini hakuwahi kuzitazama.
4. Producer huyu alikua akipigiwa simu mara nyingi lakini hakuwa anapokea na hata msg anaweza kujibu au kutojibu ambapo linah anasema ‘ilikua ngumu sana mwanzoni lakini baada tu ya kuingia studio kuweka voco ya kwanza nikapata na kolabo hapohapo, yani walikubali uwezo wangu’
Screen Shot 2014-09-01 at 1.35.21 AM5. Baada ya Uhuru kuona single ya ‘Ole Themba’ imeanza kuwa kubwa kwa kufanya vizuri kwenye Radio na TV kulitokea kama kutokuelewana kidogo kwa kuona Linah anaanza kupata hela.
6. ‘Waliitengeneza kama na wao wana haki na wimbo wenyewe lakini uzuri ni kwamba tulishasaini mkataba mwanzoni kuwa wimbo wametuuzia ni mali yetu na wala hawana haki yoyote, alietunga melody alisaini na tumemlipa so hausiki tena, tulimlipa kila mtu na kazi yake…. namshukuru Mungu iliisha vizuri’- Linah

Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu na niko tayari kukutumia wakati wowote iwe usiku au mchana iwapo utakua umejiunga na mimi kwa kubonyeza hapa >>> twitter Insta FB

Picha 7 za kilichotokea baada ya Diamond kupelekwa kwenye show saa kumi alfajiri Ujerumani.


Picha 7 za kilichotokea baada ya Diamond kupelekwa kwenye show saa kumi alfajiri Ujerumani.

Picha 7 za kilichotokea baada ya Diamond kupelekwa kwenye show saa kumi alfajiri Ujerumani.

Screen Shot 2014-09-01 at 12.16.38 AMMmiliki wa hit single ya ‘mdogo mdogo’ Diamond Platnumz anahusika tena kwenye zile habari zinazoongelewa sana ambapo time hii imetokea Stuttgart Ujerumani.
Alitakiwa kufanya show weekend iliyoisha sehemu inaitwa Stuttgart lakini ikashindikana baada ya kudai kucheleweshwa na Promota na badala yake akampeleka kwenye ukumbi saa kumi alfajiri.
Inasemekana mashabiki wenye hasira waliosubiri kuanzia saa nne usiku walianza kufanya fujo kwa kurusha chupa na kuvunja vyombo vya muziki vilivyokua vimefungwa hapo kwa madai pia kwamba vilikua vibovu ambapo inataarifiwa kwamba Ma Dj wawili walijeruhiwa kwa kiasi kikubwa pamoja na vyombo vyao kuharibiwa.
Screen Shot 2014-09-01 at 12.16.29 AMDiamond alipowasili saa kumi alfajiri tayari mashabiki walikua wametoka nje kama hivi ambapo mmoja wa mashabiki waliokuwemo kwenye tukio hilo amesema Polisi walilazimika kuingilia kati na Diamond hakudhurika.
Platnumz ambae ameahidi kuongea na Amplifaya ya CloudsFM aliandika kwenye mitandao yake ya kijamii muda mfupi baada ya hilo tukio >>>> ‘kiukweli nimesikitishwa sana na uandaaji wa kampuni hii ya BRITTS EVENTS iliyoandaa show ya Stuttgart Germany, Promoter anatupeleka kwenye show saa kumi alfajiri
Naomba mtambue halikua kosa langu, mimi ni mgeni tu na ninafata maelekezo ya Promoter hivyo nisingeweza kujiamulia kuja muda ninaotaka mimi‘ – Diamond
Screen Shot 2014-09-01 at 12.16.12 AM
Screen Shot 2014-09-01 at 12.16.04 AM
Screen Shot 2014-09-01 at 12.15.56 AM
Screen Shot 2014-09-01 at 12.16.49 AM
Screen Shot 2014-09-01 at 12.16.59 AMPicha zimepigwa na OldMombasa.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu na niko tayari kukutumia wakati wowote iwe usiku au mchana iwapo utakua umejiunga na mimi kwa kubonyeza hapa >>> twitter Insta FB

TAMASHA LA FIESTA 2014 LAWA GUMZO MKOANI TANGA.

TAMASHA LA FIESTA 2014 LAWA GUMZO MKOANI TANGA.

Vanessa Mdee a.k.a Vmoney akiimba jukwaani huku akiwa na staili yake ya kipekee kabisa
Barnaba Boy akiimba juu ya jukwaa la Fiesta ndani ya uwanja wa Mkwakwani mkoni Tanga mwishoni mwa wiki
Wadau nao walikuwepo kupata selfie ya Globu ya jamii ndani ya Fiesta.
Linah akilinogesha jukwaa la Fiesta na wimbo wake wa Ole Temba.
Kwa jijna la Kisanii anajiita Vmoney a.k.a Vanessa Mdee akiimba kwa hisia jukwaani
Ommy Dimpoz akiimbajuukwani wimbo wake wa Nani kama Mama
Ommy Dimpoz na vijana wake wakilishambulia jukwaa.
Ommy Dimpoz akimpagawisha shabiki wake jukwaani kwa staili ya Kantangazee...!
Ali Kiba na vijana wake wakilishambulia jukwaa la Fiesta
Msanii wa muziki wa kizazi ajulikanae kwa jina la Khadija Maumivu akiiimba jukwaani kwenye tamasha la Fiesta 2014 ndani ya uwanja wa Mkwakwani,mkoani Tanga lililofanyika mwishoni mwa wiki.
Anajiita Rais wa Manzese,Madee akiwaimbisha wakazi wa jiji la Tanga waliojoitokeza kwenye tamasha la Fiesha mkoani Tanga mwishoni mwa wiki.
Sehemu ya umati mkubwa wa wakazi wa jiji la Tanga waliojitokeza kwenye tamasha la Fiesha mwishoni mwa wiki.
Pichai kati ni msanii wa muziki wa kizazi kipya,Linah akiwa sambamba na madansa wake wakilishambulia jukwaa,mbele ya umati mkubwa wa wakazi wa jiji la Tanga (hawapo pichani) waliojitokeza kwenye tamasha la Fiesta ndani ya uwanja wa Mkwakwani,mwishoni mwa wiki.
Maelekezo ya hapa na pale kutoka kwa mafundi mitambo na jukwaa ilikuwa ikifanyika ili mambo yaende sawa
Umati wa watu uliofurika katika Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga kupata burudani safi wakati wa tamasha la Fiesta 2014 lililofanyika mwishoni mwa wiki.
Ilikuwa ni Sheeddaah kwa wakazi wa jiji la Tanga ndani ya uwanja wa Mkwakwani mwishoni mwa wiki.
Rachae akiiimba jukwaani.
Sehemu ya umati mkubwa wa watu ukifuatilia yaliyokuwa yakijiri ndani ya uwanja wa Mkwakwani wakati tamasha la Fiesta 2014 likiendelea
Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Rachael akionesha umahiri wake wa kucheza na kuimba mbele ya umati wa watu uliofurika katika Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga (hawapo pichani ) kwenye tamasha la Fiesta 2014 ndani ya uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga mwishoni mwa wiki
Msanii wa Muziki wa kizazi kipya, Khadija Mumivu, akikonga nyoyo za mashabiki walioingia katika tamasha la Fiesta 2014 lililofanyika katika Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga  mwishoni mwa wiki.
Kwa jina la kisanii anaitwa MO MUSIC akiwakuna wakazi wa jiji la Tanga waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Fiesta lililofanyika mwishoni mwa wiki jijini Tanga
Mmoja wa wasanii wa kundi la ngoma asili ya Baikoko toka mjini Tanga akiwajibika jukwaani wakati wa tamasha la Fiesta 2014
Umati wa watu uliofurika katika Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga kupata burudani safi wakati wa tamasha la Fiesta 2014 lililofanyoka mwishoni mwa wiki.
Sehemu ya watazamaji wakiendelea kutazama yaliyokuwa yakijiri kwenye tamasha hilo mwishoni mwa wiki mjini Tanga.PICHA ZOTE NA MICHUZIJR-FIESTA TANGA.