Official fan blog "Classmate" is one among Bongo Classmates properties... It's all about reporting of Current affairs..
Pages
▼
Pages
▼
Pages
▼
Wednesday, 28 May 2014
PICHAZ........ASKARI AUAWA KIKATILI NA MAJAMBAZI..........(TAHADHARI,PICHA ZINATISHA).
Mwili wa askari aliyeuawa ukiwa katika chumba
cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Temeke
Askari polisi mmoja wa kituo cha polisi
Chang'ombe, Mkoa wa kipolisi wa Temeke,
ameuawa kikatili siku ya ijumaa mchana baada
ya kupigwa risasi ya kifua na majambazi
waliokuwa wanajaribu kutoroka baada ya
kufanya tukio la kihalifu.
Askari hao waliokuwa doria katika eneo la Wailes
walijikuta wakishambuliwa kwa risasi na
majambazi hao mara baada ya majambazi hao
kujaribu kukimbia katika eneo la tukio kwa
kutumia usafiri wa pikipiki kipindi ambapo askari
polisi walikuwa karibu na eneo la tukio.
Hata hivyo wakati askari hao wakijaribu
kuwafukuza majambazi hao wawili kwa lengo la
kuwakamata ndipo jambazi mmoja alitoa bastola
na kumpiga risasi ya kifua askari huyo na
kufariki pale pale.
Mwili wa askari huyo ukiwa umehifadhiwa.
Hata hivyo katika harakati za kujaribu kukimbia
majambazi hao walianguka na pikipiki
waliyokuwa wakitumia ndipo wakaamua kutimua
mbio mitaani na kuingia katika nyumba moja
ambapo walijificha na kujifanya kama ni wakazi
wa eneo hilo, baada ya wananchi na polisi kufika
katika nyumba hiyo, baadhi ya majirani
waliwaambia polisi kwamba wameona watu hao
wameingia katika nyumba hiyo.
Baada ya polisi kuingia waliwakuta watu hao
wakiwa wametulia kama kwamba wao ni
wakaazi wa nyumba hiyo na wala hawajui
lililotokea.
No comments:
Post a Comment