Pages

Pages

Pages

Wednesday, 28 May 2014

PICHAZ.....AFIA GESTI,NI MTUMISHI WA IDARA YA AFYA.





Mwili wa Marehemu Munuo ukitolewa katika
Gesti hiyo
Mtumishi wa idara ya Afya katika halmashauri
ya mji wa Kahama, Mkoani Shinyanga,
Jeremiah Munuo (50) amekutwa amefariki dunia
katika nyumba moja ya kulala wageni mjini
Kahama.
Taarifa kutoka jeshi la polisi wilayani humo
zimesema kwamba Tukio hilo limetokea usiku
wa kuamkia leo katika nyumba hiyo iitwayo KK
Lodge iliyopo jirani na ofisi za Halmashauri ya
Mji wa Kahama.
Taarifa zimesema watumishi wenzake
walikwenda kumuona leo majira ya saa 6
mchana baada ya simu yake kuita bila
kupokelewa kwa muda mrefu.
Jesh la polisi wilayani Kahama limefika katika
eneo la tukio na kumkuta marehemu Munuo
ambaye alikuwa na miezi 3 tu tangu ahamishiwe
katika halmashauri hiyo akiwa na Fedha taslimu
shilingi 596,000 na simu nne za mkononi.



Mwili wa marehemu Munuo umepelekwa
kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti
cha hospitali ya wilaya hiyo na uchunguzi juu
ya tukio hilo bado unaendelea.



Mwili wa Marehemu Munuoukiwa katika chumba
cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya ya Kahama 
   


Marehemu Munuo akiwa katika gesti hiyo
alikokuwa amelala
mwili wa Marehemu Munuo baada ya kugeuzwa
na kukaguliwa

No comments:

Post a Comment