Pages

Pages

Pages

Saturday, 31 May 2014

MAMBO 6 AMBAYO WANAUME HAWAPENDI KUFANYIWA NA MADEMU ZAO.



Haya niliyapata kutoka kwa mshauri wa masuala
ya mahusiano, ndoa na vijana
 Frederick Kyara. Hizi ni baadhi tu nakuwekea
hapa japo kuna vitu pia wanawake
hawavipendi kutoka kwa wenzi wao wanaume.
Nayo ni haya hapa, ungana nam
i kujadili jambo hili ambalo kwangu nimeona ni
changamoto au niseme sikujua.

1. Wanaume hawapendi kuambiwa cha kufanya
na wenzi waoMwanamke
unapotaka mwanaume afanye jambo
usimwambie alifanye bali fanya kama
 una mpa ushauri. Kwamba John hivi kwa nini
tusiweke balbu hapa kwenye
 korido maana kuna giza kweli. Badala ya hivi
wewe John huoni hapa kwenye
korido kuna giza balbu imeungua mwezi sasa
hujabadilisha kwa nini?
 Weka balbu bwana. Atafanya au asifanye kabisa
kwa sababu umemwambia cha kufanya.

2. Wanaume hawapendi mwenzi mwenye
makelele, mlalamishiYeye ni kulalamika
kuanzia Jumatatu hadi Jumapili. Japo
wanawake nao wanasema kuna wanaume
walalamishii balaaa. Na wenye gubu wanasusa
kula mpaka kuongea wanawanunia
 wake zao mmmmh!

3. Wanaume hawapendi mwenzi mchafu Mchafu
wa mwili wake na hata
nyumbani kwenye suala la kutunza nyumba
wanayoishi. Uchafu hufanya
 mwanamke apoteze mvuto.

4. Wanaume hawapendi mwenzi mbishi Japo na
wanawake wanasema
 wanaume ndio wabishi zaidi. Utampa
mwanaume ushauri lakini haufanyii
kazi ubishi mwingi.

5. Wanaume hawapendi kuamrishwa na mwenzi
wao Mwenzi mbabe
 anaetoa amri na kumtawala hawataki.

6. Wanaume hawapendi kuhisiwa hisiwa na
kusachiwa sachiwaKumpekua
kwenye simu, mifuko ya suruali kwamba
unamulika mwizi. Hawapendi,
 tena pengine hawajafanya jambo la kuwafanya
wahisiwe vibaya.

No comments:

Post a Comment