Pages

Pages

Pages

Saturday, 31 May 2014

USIRUHUSU MAPENZI YAUTESE MOYO WAKO!



NATUMAINI hamjambo wasomaji wangu na
kama unasumbuliwa na jambo lolote, iwe kiafya
au kiuchumi naomba usikate tamaa kwani
matatizo ni sehemu ya maisha, jambo la muhimu
ni kumuomba Mungu na kujaribu kutafuta suluhu
ya tatizo hilo.
Baada ya kusema hayo, basi tuingie moja kwa
moja kwenye mada yetu kama inavyojieleza
hapo juu. Ni wazi kwamba mapenzi yanachukua
nafasi kubwa sana katika maisha ya binadamu,
na ipo dhahiri kwamba mapenzi yanaweza kuleta
furaha maishani mwako lakini wakati huohuo
yanaweza kuleta maumivu, mateso na karaha.
Watu wengi sana bado wanalizwa na mapenzi na
hii ni kwa sababu hawafuati kanuni sahihi ya
mapenzi. Ndiyo... mapenzi yana kanuni zake.Kwa
bahati mbaya kabisa, kwa sasa mapenzi
yamegeuzwa na kuwa kama kitu cha kujaribu au
kufanyia biashara na ndiyo maana yanawatesa
wengi. Lakini ni kwa nini mapenzi yaendelee
kututesa? Au ni kwa sababu hatujui maana
halisi ya mapenzi? Hebu tuyaangalie mapenzi
kwa jicho la tatu.
MAPENZI NI NINI?
Katika hali ya kawaida, mapenzi hayaelezeki
kuwa ni nini. Ni vigumu sana mtu kukueleza
maana ya mapenzi ndiyo maana kila mtu ana
uelewa tofauti juu ya suala hilo.
Mtaalamu mmoja wa masuala ya mapenzi Davis
Kurt kutoka Colombia, aliwahi kuyaelezea
mapenzi ndani ya kitabu chake cha More About
Love, ambapo alisema; ‘Love is natural feelings,
which take place from the deepest part of your
heart upon somebody or something else’
akimaanisha kuwa mapenzi ni hisia za asili
ambazo huchukua nafasi kutoka sehemu ya
ndani kabisa ya moyo juu ya mtu au kitu
chochote. Tena bila kuwa na visingizio au
masharti ya aina yoyote.
HISIA NI NINI?
Huu ni msukumo wa vichochezi katika homoni
za ndani ya mwili ambazo hutokea kutokana na
mazingira.
Lakini huwa tofauti kati ya mtu na mtu na ndiyo
maana watu hutofautiana madaraja ya kupenda.
Mfano halisi ni kwamba, utakuta mtu anapenda
sana wanawake weupe, lakini mwingine hataki
hata kuwaona.
Lakini mapenzi siyo mawazo au uamuzi wa mtu,
bali hisia ambazo hutokea pasipo uamuzi wa
mtu.
Kutokana na hali hiyo, utasikia mtu akisema
‘sijui nimempendea nini huyu mwanaume!’ ni
kweli yeye hajaamua lakini hisia zimefanya awe
hivyo.
USIRUHUSU MAPENZI YAKUTESE
Kwa nini mapenzi yakuumize? Unakosea wapi?
Kwa nini ukataliwe kila mara? Haya ni baadhi ya
maswali ya kujiuliza kuhusu mateso ya mapenzi.
Kamwe katika maisha yako usiruhusu mapenzi
yakutese, najua yawezekana kila mpenzi
unayempata haudumu naye, wewe ni mtu wa
kulia kila siku, hujawahi kufurahia maisha hataa
siku moja, jipange upya.
Thamini na jali zaidi maisha yako kwanza, fikiria
kipi ni bora kati ya mapenzi na maisha yako, ni
kipi kilitangulia? Kama maisha ndiyo yalitangulia
kwa nini usijijenge kwanza kimaisha ndipo
mengine yafuate?
Hata kama unateswa na mtu unayempenda kwa
dhati, hata kama ni mzuri kwa kiwango gani,
kwani bila yeye maisha hayaendi? Si kweli na
kama unaweza kuishi bila yeye kwa nini akutese
namna hiyo?
Usikubali hisia zako zichezewe, mwamuzi wa
mwisho wa maisha yako ni wewe mwenyewe. Ni
vyema kuchuja mambo na kuwa katika uhusiano
na mtu sahihi ambaye mnagongana kihisia.
Kama hisia zako na zake ni tofauti, kwa nini
uendelee kumng’ang’ania? Bado kuna vitu
muhimu vya kujifunza hapa,

No comments:

Post a Comment