Official fan blog "Classmate" is one among Bongo Classmates properties... It's all about reporting of Current affairs..
Pages
▼
Pages
▼
Pages
▼
Wednesday, 21 May 2014
LINEX SASA ATAKA KUHAMIA FINLAND BAADA YA KUGOMA KWA SIKU NYINGI KWENDA HUKO
Linex ambae ni staa wa single mpya ya ‘Onga
onga’ aliwahi kutangaza kupitia AMPLIFAYA ya
CloudsFM pamoja na millardayo.com kwamba
ameachana na mpenzi wake raia wa Finland
ambae walikutana kwa mara ya kwanza kwenye
ndege na baada ya ukarimu wa Linex mrembo
akadata.
Walikaa kwenye uhusiano wa kimapenzi mpaka
Linex akafikia hatua ya kumvisha pete ya
uchumba lakini safari ikafikia mwisho miezi
michache baadae baada ya mrembo huyo kurudi
Finland na kumtaka Linex amfate huko wakaishi
pamoja.
Linex alikata kuhamia Finland kwa kudai
ameteseka kwa miaka kutafuta njia ya kutoka
kimuziki Tanzania hivyo baada ya kufanikiwa
hawezi kuihama nchi na kwenda kuanza maisha
mapya kwa mara ya kwanza nje ya nchi wakati
anategemea maisha yake yaendeshwe na muziki.
Baada ya miezi kupita ya uhusiano wao
kukatika, mrembo amerudi tena kwa Linex na
kumuuliza kama ni sahihi akiendelea kuvaa pete
ya uchumba aliyomvalisha?
Linex anasema ‘haya ni maisha na unaweza
kuona umesonga mbele lakini inafikia time kuona
ulikosea hivyo unataka kurudi nyuma na ni
wachache sana huwa wanafanikiwa kurudisha
siku nyuma, mi sikumchunia nilikua nachat nae
na kuwasiliana wakati wote ila juzi kanipigia
simu ananiomba kwa kuuliza bado anaweza
kuendelea kuvaa ile pete ya uchumba?’
‘Nilimvisha pete ya uchumba na akawa ndio
Mwanamke wa kwanza kumvisha na ikawa ishu
kubwa baada ya wazazi wangu kufahamu
wakakasirika kwa sababu sikuwashirikisha…. so
mrembo ananiuliza anaweza kuivaa ile pete kwa
misingi ile niliyokua naitaka wakati namvalisha?
bado sijapata maamuzi so nilimwambia hiyo
haiwezi kuwa rahisi hivyo’
‘Amekua akiniuliza kama nimepata mpenzi
mwingine na jibu langu ni hapana sijapata
ambapo baada ya kuona nimekua mzito kutoa
jibu kuhusu uvaaji wa pete hiyo ameamua kuja
Tanzania mwisho wa May 2014 ili tuongee, sijui
nitaongea nini kwa huyu mwanamke ambaye
kiukweli ni wa tofauti kukutana nae maishani
mwangu, nikimuelewa nitarudiana nae tu kwani
watu wangapi wamerudishaga majeshi kwa
wapenzi wao wa siku nyingi?’
Pamoja na kuyasema hayo, Linex amesema bado
anaudai huu muziki wa bongofleva na ili aweze
kupata hela ni lazima afanye kazi sana na
msimamo wake wa kutohama Tanzania uko
palepale… ‘siwezi kuuacha huu muziki
ulionifanya nitembee juu ya treni sina nauli
natoka Kigoma naufata Dar, huwezi kuningo’a
Tanzania hivihivi yani… Ulaya siku hizi ni
pakwenda kutembea na kurudi tu’
Unadhani msimamo wa Linex ni sahihi?
ungempa tena nafasi mpenzi wako baada ya
kukuacha kwa miezi?
No comments:
Post a Comment