Pages

Pages

Pages

Wednesday, 21 May 2014

BIFU LA WEMA NA KAJALA SASA KUFIKIA BUNGENI.





Ule mgogoro wa mastaa wawili ambao wote ni
waigizaji wa filamu nchini Wema Sepetu na
Kajala Masanja umefika kwa waheshimiwa
wabunge ambao wamewataka mastaa hao
wawili kukaa chini na kumaliza tofauti zao na
kuwa mashostito wa kutupwa kama awali. Kwa
mujibu wa chanzo kimoja makini kikizungumza
na Globapublishers wabunge hao ambao wengi
wanapenda sanaa wamemwambia kiongozi wa
kundi la Bongo Movie Unity Steve Nyerere afanye
juu chini Wema na Kajala wamalize ugomvi wao
na kama akishindwa basi awaambie ili wao
wawakalishe chini kwa kuwa wasanii hao wana
majina makubwa na kuna chipukizi wengi
wanawangalia ili kufikia walipo hivyo haileti
picha nzuri kwa kuwa huko mwanzo walikuwa
marafiki wazuri na mfano wa kuigwa.




"Walimwambia Steve kwamba ni kitendo cha
aibu kwa mastaa wakubwa kama hao
kugombana, hiyo inawapunguzia heshima kwani
hiki kilikuwa ni kipindi cha kushikamana kwa
umoja ili kuisogeza mbele tasnia yao badala ya
kulumbana" kilisema chanzo hicho.
Nae Steve Nyerere alipotafutwa na GPL alikiri
waheshimiwa wabunge kumwambia suala hilo.


No comments:

Post a Comment