Kama ulikua na mpango wa kusafiri tarehe 11 mwezi wa saba hadi tarehe
23 basi inabidi uicheki tena ratiba yako kwani Mh. Jakaya Mrisho Kikwete
ameshafanya yake akiwa ziarani nchini marekani na kufanikisha mpango wa
kumleta mkali wa RnB Usher Raymond.
Nyota huyu ambaye anatamba kwasasa na kibao chake cha “good kisser
ataongozana na Terrence Jenkins au unaweza kumuita Terrence J ambaye ni
muigizaji maarufu wa filamu, model na pia alikua akitangaza kipindi cha
106 & Park kabla ya Bow Wow kuchukua mikoba yake.
Pia kunauwezekano wa nyota mwingine wa R&B , Trey songz naye
akadondoka naye japokua ujio wa Trey haujawa confirmed. Matamasha haya
ni mpango endelevu wa raisi kikwete kuwasaidia wasanii wetu wa
kitanzania.
No comments:
Post a Comment