Official fan blog "Classmate" is one among Bongo Classmates properties... It's all about reporting of Current affairs..
Pages
▼
Pages
▼
Pages
▼
Friday, 13 June 2014
MWANAMUZIKI WA INJILI HAPPY KAMILI, AWEKWA JELA KWA MIEZI MITATU MBEYA.
Habari za Uhakika zilizopo mjini Mbeya
zinasema kuwa Mwanamuziki wa Injili nchini
Tanzania anayejulikana kwa jina la Happy
Kamili anayetamba sana na wimbo wake
"Mpango Wa Mungu" na "Jina Kubwa"
amehukumiwa kifungo cha Miezi Mitatu Jela
bila faini katika Mahakama Ya Mwanzo Mkoani
humo kwa Kosa la Kusababisha ajali ya
barabarani.
Kesi hiyo iliyokuwa imeanza kusikilizwa mwezi
January Mwaka huu, siku ya jana imetolewa
hukumu kwa Mwanamuziki huyo kupatikana na
hatia ya kusababisha ajali kwa kugonga gari
lingine kwa nyuma. Mwanamuziki huyo baada
ya Kukiri kutenda kosa hilo mahakamani
alipatikana na hatia ya Hakimu alitoa Hukumu
ya Miezi Mitatu Jela pasipo kutoa Hukumu
Mbadala ya Faini.
No comments:
Post a Comment