Pages

Pages

Pages

Sunday, 29 June 2014

LINAH AWASILI DAR.AONGELEA KOLABO YAKE NA UHURU NA DJ MALVADO SOUTH AFRICA.



Linah amerudi Dar! ameongea kuhusu kolabo na Uhuru na Dj Malvado South Africa

DSC_0478 #1
Linah akiwa uwanja wa ndege Dar es salaam alipowasili akitokea Johannesburg South Africa ambako unaweza kwenda Jumatatu Jumatano na Ijumaa kupitia @fastjet
Katikati ya June 2014 Linah alizungumza na millardayo.com akiwa South Africa na kuthibitisha kwamba kilichompeleka huko na kumfanya akae kwa zaidi ya siku 20 ni kazi ya muziki.
Miongoni mwa alivyokua anavifata ni kufanya kolabo na Oskido staa wa muziki wa Afrika kusini ambae ndio anawasimamia Mafikizolo ambao pia wanarekodi kwenye studio yake.
linah122Baada ya kutua Dar es salaam akitokea Johannesburg, Linah ameithibitishia millardayo.com kwamba tayari amefanya kolabo na kundi la Uhuru ambao walishirikishwa kwenye wimbo wa ‘khona’ na Mafikizolo.
Kwenye studio ya Oskido, palepale wanaporekodi mastaa wengine kama Mafikizolo wenyewe na Davido pia alierekodia hapo kolabo na Mafikizolo, Linah ndio amerekodi hiyo kolabo na kundi la Uhuru.
DSC_0503Wimbo wake umefanywa na producer kutoka pia kwenye kundi hilohilo la UHURU ambae ndio amehusika vilevile kwenye kolabo ya Mafikizolo na Diamond Platnumz.
35Kolabo alizorekodi South Africa ni mbili ikiwemo moja aliyoshirikishwa na Dj Malvado ambae yupo kwenye ile hit ya ‘Atchu tchutcha’ ambapo pia Linah amethibitisha kwamba kwa kipindi chote cha zaidi ya siku 20 Afrika kusini, amerekodi video na God father Director ambae amefanya video nyingi kubwa za Afrika zikiwemo za P Square, Davido, Diamond na wengine.
34

No comments:

Post a Comment