Official fan blog "Classmate" is one among Bongo Classmates properties... It's all about reporting of Current affairs..
Pages
▼
Pages
▼
Pages
▼
Wednesday, 28 May 2014
SABABU ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME.
SABABU ZA KUPUNGUKIWA NA NGUVU ZA
KIUME
Kesi ya wanaume kupungukiwa nguvu za kiume
zimezidi kushika kasi, kiasi cha kufanya dawa
za kuongeza nguvu hizo kuwa maarufu na
zenye mahitaji makubwa katika jamii.
Waganga wa kienyeji wamekuwa wakitumia
dawa hizo kama tiba ya msingi ya kuwavutia
wateja kwenye biashara zao. Hii inaonesha
kuwa tatizo hili ni kubwa miongoni mwa
wanaume wengi katika jamii yetu.
Hata hivyo, utafiti unaonesha kwamba wengi
kati ya wanaume waliowahi kutumia dawa za
asili na zile za hospitali kuondokana na tatizo la
upungufu wa nguvu za kiume hawakufanikiwa
kupata tiba ya kudumu, matokeo yake
wamegeuzwa kuwa watumwa wa kila
wanapotaka kushiriki tendo lazima wabwie
‘kolezo’ la kuwasaidia kuamsha hisia zao.
Kwa wanaume, ukosefu wa nguvu ni jambo
linalouma na kuondoa kabisa ujasiri. Wengi kati
yao wako tayari kutumia pesa na uwezo wao
wote kuhakikisha kuwa heshima ya tendo la
ndoa inakuwa katika miliki yao daima.
Lakini, watafiti wa masuala ya mapenzi
wamegundua kuwa wengi kati ya hao
wanaolalamika kupungukiwa nguvu za kiume,
hawafahamu chanzo cha matatizo na namna
wanavyoweza kuepukana na kasoro hizo.
Ushahidi uliopatikana kwa waathirika wa tatizo
hili, unaonesha kuwa wanaume wanapokabili
upungufu wa nguvu za kiume huishia kujuta na
kujilaumu wenyewe bila kutazama upande wa
pili wa washirika wao, namaanisha wanawake.
Zipo kesi za wanaume kujiua au kujinyofoa
sehemu zao za siri kwa sababu ya kushindwa
katika tendo la ndoa. Hali hii inatoa picha
kwamba wanaume wengi hujitwika mzigo wa
lawama wenyewe.
Dokta Bianca P. Acevedo kutoka Chuo Kikuu
cha California, Santa Barbara anasema,
wanawake huchangia kwa kiasi kikubwa tatizo
la upungufu wa nguvu za kiume, jambo ambalo
nami nalithibitisha kwa ushahidi wa kitaalamu
ufuatao:
1: KAULI
Miongoni mwa mambo ambayo mwanaume
hataki kuyasikia yakitoka kwenye kinywa cha
mwanamke ni kuambiwa HAWEZI TENDO LA
NDOA. Mwanamke akimwambia mwanaume
wakati au baada ya tendo kuwa hawezi,
atakuwa amemsababishia tatizo kubwa la
kisaikolojia ambalo litampelekea kupotea nguvu
za kiume taratibu.
Msaada unaohitajika kwa mwanamke
anayekutana na mwanaume dhaifu kwenye
tendo si kumwambia hawezi, bali ni kumtia
moyo na kumsaidia kuweza. Wanawake
wamewasababishia waume zao upungufu wa
nguvu za kiume kwa kuwaambia maneno kama
haya: “Yaani siku hizi sijui umekuwaje, yaani
huwezi kazi kabisa!”
2 : UJUZI
Wanawake wengi hasa waliopo kwenye ndoa,
wanapuuza ujuzi kwenye tendo la ndoa.
Hawajishughulishi kumsaidia mwanaume
‘kuwika’, si wabunifu na watundu, jambo hili
humfanya mwanaume kushiriki tendo kwa
kutegemea kupanda kwa hisia zake mwenyewe,
hivyo anapokuwa amechoka au ana mawazo,
hawezi kusisimka kwa vile hapati ushirikiano
toka kwa mwenzake.
Pamoja na wengi kutokuwa wajuzi, lakini wapo
wengine ambao ni watundu mno kwenye sita
kwa sita kiasi cha kumfanya mwanaume ajione
kama mgeni wa mchezo huo.
Kimtazamo, wanaume hupenda sana ushindi
wakati wa ‘kazi’, lakini pale wanapogeuzwa
‘chekechea’ hupunguza uwezo wa kujiamini na
kuruhusu hofu kuongezeka mawazoni mwao,
hivyo kuwasababishia tatizo la upungufu wa
nguvu za kiume.
Inashauriwa kwamba, mwanamke anapokuwa
na uelewa mkubwa wa masuala ya mapenzi
hasa wakati wa tendo, asioneshe kiwango
kikubwa kwa haraka bali amchukulie mwenzake
kama mwanafunzi, asiwe na maneno kama:
“Leo nakuja kukupa vitu adimu kuliko vya juzi,
hakuna kulala kasi mtindo mmoja.” Kauli hizi
huwaogopesha wanaume na kuwafanya
wapungukiwe na nguvu.
3.USAFI
Mwanamke anapokuwa si msafi, huweza
kumsababishia mwanaume matatizo ya
upungufu wa nguvu za kiume. Sote tunafahamu
umuhimu wa usafi wa mwili na kero za uchafu
wakati wa tendo, hivyo ni wazi kuwa
mwanamke akiwa mchafu atamfanya
mwanaume apoteze msisimko na uwezo wa
tendo la ndoa. Unadhifu wa mavazi na mwili ni
muhimu sana katika mapenzi.
4.GUBU
Jambo lingine linaloweza kumsababishia
mwanaume upungufu wa nguvu za kiume ni
gubu au karaha za maneno ya uchokozi
yasiyokuwa na kichwa wala miguu. Uchokonozi
wa mambo, ugomvi, usaliti na hali ya kutokuwa
na staha ni mambo yanayosababisha tatizo la
upungufu wa nguvu za kiume.
Mwanamke anapokuwa mwingi wa maneno ya
kashfa, dharau na matusi huweza kumfanya
mume amchukie na kutopenda kushiriki naye
tendo. Uchunguzi unaonesha kwamba
wanawake walioolewa wenye tabia hii,
huwafanya waume zao wawe na msisimko wa
kimapenzi kwa wanawake wa nje kuliko wake
zao hao.
5.USALITI
Tabia ya usaliti kwa mwanamke ni chanzo
kingine cha mwanaume kupata tatizo la
upungufu wa nguvu za kiume. Mwanaume
anapoona, kuhisi au kubaini kuwa anasalitiwa,
huumia sana moyoni, maumivu ambayo
hatimaye humfanya muhusika kuwa na mawazo
mengi ambayo humuondolea hamu ya tendo.
Mada hii imezungumzia zaidi wanawake, lakini
vipengele vilivyomo kwenye somo hili
vinatumika pia kwa upande wa wanaume
kuwasababishia wanawake matatizo ya
kupoteza msisimko wakati wa tendo.
PIA
WANAWAKE WAMECHANGIA TATIZO LA
UKOSEFU WA MBEGU ZA KIUME KWA ASILIMIA
100 ........
HII NI KUTOKANA NA TABIA YAO YA KUANIKA
VIUNGO NYETI HADHARANI KAMA MATITI,
MAKALIO YAO NA MAPAJA..........
ZAMANI ILIKUWA KWAMBA UKILIONA PAJA LA
MWANAMKE, NI LAZIMA USISIMKE.......
.WALIOZALIWA MIAKA YA 80 NA KURUDI
NYUMA WANAJUA.......
LEO HII TUNAKAA NA WADADA WAKIWA NUSU
UCHI, MIPAJA YAO IKIWA NJE NJE KIASI
KWAMBA TUMEFIKIA HATUA TUNAONA NI
JAMBO LA KAWAIDA SANA........
NI UKWELI USIOPINGIKA KUWA WANAWAKE
WAMEWAHARIBU SANA WANAUME
KIHISIA.....PAMOJA NA JITIHADA ZOTE
ZAKUWASEMA NDO KWANZA WANAONGEZA
VITUKO
HAPA NI KUMKUFURU MUNGU.......ACHENI
MAMBO YA KUIGA......NIKUJIDHALILISHA.
No comments:
Post a Comment