Pages

Pages

Pages

Saturday, 17 May 2014

JB AINGIZWA MKENGE NA WEMA SEPETU, AUNT EZEKIEL.




IMEKULA kwake! Wauza nyago kwenye sinema
za Kibongo, Wema Isaac Sepetu na Aunt Ezekiel
Grayson wamemuingiza mkenge staa mwenzao,
kaka mkubwa Jacob Steven ‘JB’ baada kukubali
mwaliko kisha kumkatalia dakika za mwisho.



Staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac
Sepetu.

Habari za ndani zilidadavua kwamba JB na
wasanii hao walitakiwa kusafiri kwenda nchini
Uturuki kwa ajili ya kujifunza utamaduni wa huko
ambapo walipelekwa na uongozi wa Ukumbi wa
Princess Cassino uliopo Posta jijini Dar.
Katika hali ya kushangaza, uongozi huo ukiwa
tayari umeshawakatia tiketi za daraja la kwanza
(first class) zinazogharimu kama dola elfu moja
(zaidi ya Sh. milioni 1.6) kila mmoja na baadhi
ya wasanii kama Vincent Kigosi ‘Ray The
Greatest’ na Amri Athuman ‘Mzee Majuto’, Wema
na Aunt Ezekiel walikataa siku moja kabla ya
safari.



Diva kwenye tasnia ya filamu Bongo, Aunt
Ezekiel Grayson.
Chanzo chetu makini kilipenyeza habari kuwa,


Wema na Aunt walichomoa safari hiyo baada ya
kuhisi haikuwa na maslahi kwao na
walivyopeleka maombi yao ya kimaslahi kwa JB,
aliwaambia ni safari ya kujifurahisha na hakuna
fedha yoyote watakayopata.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, Risasi
Jumamosi lilimtafuta Aunt ambaye alikiri
kuchomoa safari hiyo baada ya kushindwana
kimaslahi.

“Unajua ile ni kwenda kutangaza biashara ya
mtu kwa hiyo sisi tuliwatajia kiasi cha fedha
ambacho tulikitaka kulipwa lakini tulishindwana
ndiyo maana tukakataa kusafiri maana hatuwezi
kufanya kitu ambacho hakina maslahi kwetu na
kwenda kuwafaidisha wengine,” alifunguka Aunt.

Naye Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven
Mengere ‘Nyerere’ aliilaani safari hiyo na
kusema kwamba JB ni mnafiki kwani
aliwachagua wasanii wachache kwa upendeleo
ambao baadhi yao wamemwangusha kwa
kutokwenda.

“Ukweli nimegundua JB ni mbinafsi, nilikuwa
naambiwa lakini nikawa namtetea, sasa
nimeamini kwamba hafai akirudi lazima
nitamuita, nitazungumza naye kwa nini aliamua
kufanya hivyo wakati kila kitu kinapotokea iwe
safari au vitu vingine huwa sisi Bongo Movie
Unity tunashirikishana lakini kwa hili ameona
afanye mwenyewe,” alisema Steve Nyerere.


CREDIT:PAMOJASISI BLOG.
                (FRANCIS MASHALLA)

No comments:

Post a Comment