Pages

Pages

Pages

Wednesday, 12 November 2014

TCRA YAWATAKA WAMILIKI WA BLOGS TANZANIA KUZITUMIA VIZURI WAKATI WA UCHAGUZI



WAMILIKI wa Blogs nchini
wametakiwa kuzitumia
vyema blog zao katika
kuripoti habari na matukio
mbalimbali wakati wa
uchaguzi wa serikali za
mitaa, wabunge na urais.
Hayo yamesemwa na
Mkurugezi Mkuu wa
Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania (TCRA), Profesa
John Nkoma leo alipokuwa
akizungumza na wamiliki wa
Blogs hizo katika Ukumbi wa
Mlimani City jijini Dar es
Salaam.

Profesa Nkoma alisisitiza
kwamba wakati wa uchaguzi
wamiliki wa Blogs
wanatakiwa kutoa fursa
sawa kwa kila upande
pasipo upendeleo wowote
wala uchochezi.

Aidha katika mkutao huo,
wamiliki wa Blogs
walikubaliana kuendeleza
mchakato wa kuwa na
umoja wao uliosajiliwa
kisheria ambapo walichagua
viongozi wa muda
watakaosimamia mchakato
huo.
Uongozi wa muda
uliopitishwa na wamiliki hao
ni kama ifuatavyo:

1.Joachim Mushi -
Mwenyekiti

2. Francis Godwin - Makamu
Mwenyekiti

3. Khadija Kalili - Katibu

4. Shamim Mwasha -
Mjumbe

5. Othman Maulid - Mjumbe

6. William Malecela
'Lemutuz'- Mjumbe

7.Henry Mdimu - Mjumbe

TCRA imeahidi kutoa
ushirikiano katika mchakato
huo wa kusajili umoja wa
wamiliki wa Blogs na kutoa
elimu katika masuala
mbalimbali yatakayosaidia
jamii.


CREDIT: UDAKU SPECIALLY.

No comments:

Post a Comment