BIBI KIZEE AJIANDALIA JENEZA!
Mkazi wa Kijiji cha
Lundusi, Kata ya Peramiho, wilayani Songea, Mkoa wa Ruvuma, Bibi
Scholastica Mhagama amejiandalia jeneza lake ambalo litatumika kumzikia
siku atakayoaga dunia.
Akizungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki iliyopita, Scholastica
alisema alilitengeneza jeneza hilo zaidi ya miaka mitano iliyopita baada
ya kuona anaishi kwa dhiki na anatengwa na baadhi ya watu.
“Nilijitengenezea jeneza langu na fundi alipomaliza kazi, niliingia ndani kupima kama ninatosha, nikajilaza na kuona liko sawasawa,” alisema bibi huyo.
“Nilijitengenezea jeneza langu na fundi alipomaliza kazi, niliingia ndani kupima kama ninatosha, nikajilaza na kuona liko sawasawa,” alisema bibi huyo.
Akifafanua zaidi bi mkubwa huyo alisema ameishi maisha ya dhiki na
kunyanyaswa bila msaada kutoka kwa jamii anayoishi, hali ambayo
imemfanya amuombe Mungu amchukue ili azikwe kwenye jeneza
alilojiandalia.
“Kila siku naomba Mwenyezi Mungu anichukue haraka ili nikapumzike
kutokana na mateso ninayoyapata, lakini hofu yangu ilikuwa je nikifa,
nitazikwa kama binadamu wengine? Ndiyo maana nimeamua kujiandalia jeneza
langu,” alisema bibi huyo mwenye ulemavu wa mguu uliotokana na
kung’atwa na nyoka kisha kukatwa huku mwingine ukimsumbua kukunjuka.
Alipoulizwa sababu ya kutengwa na jamii, bibi huyo alisema: “Nimetengwa
na jamii na majirani wanashindwa kunisaidia wanadai eti mimi ni mchawi
kwa sababu watoto wangu wote wanne walikufa wakiwa wadogo. Naumia sana
kusingiziwa kitu ambacho sikijui.’’
Bibi huyo anayeishi katika kibanda kilichoezekwa kwa nyasi anasema kuwa,
aliweza kutengeneza jeneza hilo baada ya kupewa shilingi 40,000 na
mfadhili mmoja.
“Tayari nilikuwa na mbao, hivyo kazi ilikuwa kumlipa fundi fedha na
kumpa mbao ili anitengenezee jeneza,” alisema Scholastica. Bibi
Scholastica akiwa nje ya nyumba yake siku alipoongea na mwandishi wetu.
No comments:
Post a Comment