AUNT ALIANGUSHIA MAOMBI PENZI LA DIAMOND, WEMA
KUTOKA moyoni? Staa
wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel amefunguka kuwa siku zote amekuwa
akimuombea dua shosti wake, Wema Sepetu ‘Madam’ na mwandani wake, Nasibu
Abdul ‘Diamond’ uhusiano wao udumu.
Aunt alifunguka hayo mara baada ya kuulizwa na mwanahabari wetu juu ya
mtazamo wake kuhusu mapenzi ya wawili hao ambapo alisema mapenzi yao
yamekuwa yakimvutia na kila mmoja anaonekana kuwa na mapenzi ya kweli
kwa mwenzake hivyo hawezi kupendezwa hata siku moja akiona hawapo
pamoja.
“Kusema kweli naona hawa watu wanapendana na kujaliana sana, siku zote
nawaombea kwa Mungu mapenzi yao yadumu milele na ninaamini watafikia
malengo yao, sitapenda hata siku moja kuona wapo tofauti,” alisema Aunt.
No comments:
Post a Comment