Pages

Pages

Pages

Wednesday, 11 June 2014

TATOO ZA WASANII WA BONGO NA MAANA ZAKE.

Kama tungekua nchi za wenzetu tukaanza
kuandika kuhusu tatoo na wasanii basi
tusingemaliza leo maana karibia kila msanii ana
tatoo na sio moja tu bali zaidi ya moja.Lil
Wayne ana zaidi ya tatoo 300 , Rihanna ana
tatoo 19 ,Miley Cyrus ana tatoo 19 pia huku
Bruno Mars akiwa na Tatoo 5 . Lakini vipi kwa
upande wa bongo , Tatoo na usanii au umaarufu
vimeanza kuendana hapa bongo na hii ni list ya
wasanii wa bongo wenye tatoos.

Diamond Platnumz
Diamond ana tatoo kubwa kwenye mkono wake
wa kulia maeneo ya begani na nyingine kwenye
mkono wake wa kushoto yenye maandishi ya
kichina ambayo maana yake ni “I love my
mama”.


Wema Sepetu
Wema Sepetu ni moja kati ya wasanii wa bongo
wenye tatoo nyingi , ana tatoo kwenye shingo
yake , pia ana tatoo yenye maandishi ya kichina
mgongoni yenye maana ya potential kwa
kiingireza. pia ana tatoo mkononi na kwenye
bega.


Ney wa Mitego
Ney wa Mitego ni mmoja kati ya wasanii wabishi
wanaofanya muziki mgumu maarufu kama Hip
Hop, ambaye amejaribu kubeba dhana hiyo kama
msanii anayetafsirika kimwonekano. Ney wa
mitego ameanza kuchora tatoo tokea mwaka
2002 alipokua kidato cha pili katika shule ya
sekondari ya mbezi beach.Katika mkono wake
wa kulia kuna tatoo yenye nanga ya hip-hop
ikiwa na maana kuwa yeye ni mtu mwenye imani
na ndoto za kufanikiwa kupitia muziki huo wa
‘Hip Hop’.‘tattoo’ iliyopo katika mkono wa
kushoto ni nyoka mwenye mabawa
(Dragon) ,kiumbe ambacho ni adimu kuonekana
duniani.


Elizabeth Michael “Lulu”
lulu naye hayupo nyuma katika kuchora tatoo.
kwa upande wa lulu ni kidogo na wengine kwani
yeye ameambua kwenda straight forward na
kuweka ujumbe wa maneno chini kidogo ya
shingo lake karibia na bega unaosema “Only God
can Judge Me”.


Jux
Jux ana tattoo mbili. Ya kwanza ipo kifuani na
watu wengi wamekuwa wanasema tatoo hii
inafanana na ile ya trey songs lakini ukweli ni
kuwa sehemu ya mwili aliyoichorea ni kama ya
Trey Songz lakini fonts na ujumbe ni tofauti
kwani tattoo ya trey songz ameandika
ameandika kwa ajili ya mama yake , mdogo
wake wa kiume na bibi yake huku kwa upande
wa jux ukiwa na ujumbe mzito pia lakini
hatujajua bado unamhusu nani na part ya tattoo
hiyo inasema “always missing you” na “hope to
see you”. Jux ana tattoo nyingine mkononi
maeneo ya bega ikiwa na “Virgo Angel” kwa
kibongo tunaweza kuita mashuke .


Irene Uwoya
Uwoya nae ni kati ya wasanii wakubwa
wakwanza kabisa kunyesha tatoo zake. ana
tatoo juu kidogo ya matiti yake yenye alama ya
nyayo za paka au chui.Pia ana tattoo mgongoni
iliyoandikwa krrish ikiwa na alama za nyayo ya
mtoto mdogo ambayo ni maalumu kwa mtoto
wake Krrish Ndikumana.Kuna tattoo nyingine
zinaonekana kiunoni na miguuni pia.

No comments:

Post a Comment