Pages

Pages

Pages

Tuesday, 3 June 2014

TATIZO LA WANAUME KUWAHI KUFIKA KILELENI (PRE MATURE EJACULATION).

WIKI iliyopita nilifungua somo muhimu sana kwa
wanaume ambalo ni tatizo la wanaume kuwahi
kufika kileleni au kuwahi kumaliza katika tendo
la ndoa ikiambatana na uchovu wa ghafla wa
kushindwa kurejea katika tendo na mbaya zaidi
usingizi pia huwakumba ghafla wakiwaacha
wenza wao bado na hisia kali za mapenzi.
Nilisema ninaliita hili kuwa ni janga la kitaifa
kwa kuwa kliniki kwangu nimekuwa nikipokea
wanaume wengi wenye tatizo hili lakini sababu
ya pili ya kuliita janga la kitaifa ni kuwepo
wanaume wengi wenye tatizo hili lakini hawajui
kama ni ugonjwa kama yalivyo magonjwa
mengine, lina vyanzo vyake na tiba kamili kwa
hiyo wengi wao hubaki na tatizo hili likiwatafuna
mpaka uzeeni.
Niliishia kwenye vyanzo na nilianza kwa kusema
kwamba:



1. Kujichua (masturbation ) ni chanzo kikubwa
cha tatizo hili kwa kuwa mara nyingi mtu
mvulana anapoanza mchezo huu huwa anafanya
kwa siri na huhitaji amalize mapema kabla
hajakutwa na watu na tabia hii hujijenga
kisaikolojia na kujikuta mvulana/mwanaume
huyu huendelea na tatizo hili la kuwahi kumaliza
hata katika tendo halisi.
Madhara haya ya kujichua huambatana na uume
kusinyaa, kuwa mfupi na mwembamba tofauti na
awali. Tafiti za kitabibu zinatabanaisha kwamba
kila mwanaume aliyewahi kujichua mfululizo
katika maisha yake ni lazima atakumbwa na
tatizo hili kipindi fulani cha maisha yake.

2. Msongo wa mawazo. Wanaume wengi hasa
wa mijini hujikuta katika msongo wa mawazo
usiokwisha na hivyo hurudi nyumbani kutoka
katika shughuli zao za kila siku.

3. Kukamia kupita kiasi.

4. Uoga/kutojiamini. Hali hii huwakumba
wanaume wasio na taarifa kwamba wao ni
wakamilifu, wanaume ambao hujidharau na
kujiona hawafai kuwa na mwanamke wa hadhi
fulani

5. Dr. Abrahams James wa Saint Magreth Clinic
iliyopo Washington Dc katika andiko lake liitwalo
`Sex and Fertility` la mwaka 2011,
amesisitiza kwamba wanaume kutofuatilia
majarida /elimu au taarifa za mbinu mbalimbali
za kumwezesha mwanaume kuchelewa kufika
kileleni, huchangia kuendelea kwa tatizo hili kwa
kizazi na kizazi na hasa kwa wanaume wa mijini
ambao wengi wao miili yao haifanyishwi
mazoezi kwa kazi zao au hata kwa kupanga
muda.
Anasisitiza kwamba mwanaume anapopata
ufahamu huu hupata hali ya kujiamini na hivyo
kushiriki kikamilifu katika tendo la ndoa.

6. Ulaji mbovu ukiambatana na uzito kupita
kiasi.Ulaji wa siku hizi hasa mijini ni mbovu kwa
maana ya kwamba watu hujali rangi na ladha na
si viini lishe vilivyomo na pia hawajali matokeo
mabovu ya ulaji huo. Inashangaza kuona
wasomi wengi na watu wenye uwezo kifedha
wakiongoza kwa ulaji mbovu unaosababisha
pamoja na mambo mengine, kukumbwa na tatizo
la wanaume kuwahi kufikia mshindo na
kutoweza kuendelea mpaka masaa mengi au
hata siku zaidi ya moja zipite.

7. Kutofanya mazoezi na mwili kuwa legevu bila
stamina ya kutosha. Inashangaza kuwaona watu
wenye uzito mkubwa kupita kiasi au wazee au
wagonjwa ndio wapo mazoezini asubuhi na jioni.
Hiki ni kiashiria kwamba watu hufanya mazoezi
pindi wanaposhauriwa na daktari kwamba hiyo
ndiyo suluhu ya wao kuendelea kuishi ilhali
mazoezi yanapaswa kuwa sehemu ya maisha ili
pamoja na faida zingine, yawasaidie wanaume
kuchelewa kufika kileleni hasa wale ambao bado
hawajakumbwa na tatizo hili.

No comments:

Post a Comment