Pages

Pages

Pages

Saturday, 7 June 2014

PICHAZ......KIJANA ALIYEPOTEA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA APATIKANA.

Kijana mmoja mkazi wa kijiji cha Nyambogo
wilayani Rorya mkoani Mara, ambaye anadaiwa
kupotea nyumbani kwa imani za kishirikina
hatimaye amepatikana huku akiwa katika hali
ya kutisha bila kujitambua na mwili wake ukiwa
umejaa tope jingi, tukio ambalo limevuta mamia
ya wananchi wa kijiji hicho. Kijana huyo Kenedy
oguko mwenye umri wa miaka 22 amekutwa nje
ya nyumba yao asubuhi ya Juni 5 mwaka huu
akiwa uchi wa mnyama,ambapo baadhi ya
mashuhuda wa tukio hilo wamedai kuwa tangu
kutoweka kwa kijana huyo siku nne
zilizopita,wamekuwa wakimtafuta bila
mafanikio huku wakihusisha tukio hilo na imani
za kishirikina.





Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM wilaya ya
Rorya Bw Samwel Kiboye,ambaye ni miongoni
mwa mashuhuda wa tukio hilo amewaomba
wananchi kuacha kulipiza visasi kwa kuwasaka
watu wanaotuhumiwa kwa ushirikina bali
watumie vyombo vya dola huku mwenyekiti wa
kijiji hicho akilaani vikali vitendo hivyo vya
ushirikina vinavyoendelea kijijini hapo hatua
ambayo amesema imesabisha wananchi sasa
kuishi kwa hofu kubwa.
Hata hivyo katika hali ya kushangaza wazee wa
jadi kijijini hapo waliagiza kila mwananchi
kupita mbele ya kijana huyo na kumpa mkono
kama njia moja wapo ya kuwezesha kupata
fahamu kitendo ambacho hata hivyo hakikuzaa
matunda.

No comments:

Post a Comment